The House of Favourite Newspapers

SO SMART! ALICHOKISEMA VEE MONEY KWA WATOTO YATIMA

Vanessa Mdee ‘Vee Money’

UKIZUNGUMZIA wanadada wanaofanya vizuri kwenye Bongo Fleva ni Vanessa Mdee ‘Vee Money’. Amefanya mambo mengi kwenye gemu la Bongo Fleva.  Vee Money, mbali na kufanya vizuri na nyimbo kali zikiwemo Chausiku na Cash Madame, pia amepiga kolabo nyingi na wasanii wakali ndani na nje ya Bongo. Yupo kwenye uhusiano na Juma Mussa ‘Jux’, lakini pia anamsapoti mdogo wake Mimi Mars ambaye naye anafanya Bongo Fleva.

MSIKIE VEE MONEY

Over Ze Wikenda, imepiga stori na Vee Money kuhusu kazi zake kwa sasa na projekti mbalimbali, bonyeza hapa chini kusikia alichosema;

Over Ze Weekend: Umemaliza ‘Love and Money Tour’, nini kinaf-uatia baada ya ha-po?

Vee Money: Plani ni kubwa na nyingi kiukweli. Unajua kwenye muziki mafanikio hayawezi kuja hivihivi, lazima utoe jasho ili kufanikiwa.

Over Ze Weekend: Jux anakusapoti sana kwenye kazi zako, ni kwa sababu ni mpenzi wako au kwa sababu mna ‘chemistry’ kwenye kazi?

Vee Money: Ni kweli ananisapoti sana. Ukiangalia tumefanya mambo mengi pamoja, tumeshirikiana kwenye nyimbo nyingi mpaka kuja kwenye hii tour tuliyomaliza na bado kuna mengi tutafanya pamoja. Naweza kusema tunasapotiana kwa sababu ni wapenzi, lakini pia kuna chemistry ambayo mashabiki wetu wanafurahia kuisikia.

Over Ze Weekend: Mashabiki wanakusapoti kwenye kazi zako, kwa upande wako ni mambo yapi umefanya kwenye jamii kurudisha fadhila?

Vee Money: Nina projekti yangu ya Udada Talks na nimetembelea shule mbalimbali. Nilianza na Shule ya Wasichana ya Arusha, tumefanikiwa kuwapelekea umeme wa sola kwa sababu walikuwa na tatizo la umeme, lakini sasa hivi sola inawaka na wanafunzi wanaendelea na kujisomea kwa kuwa tatizo la mwanga usiku tena kwao hamna.

Over Ze Weekend: Kuna sapoti unapata nje ya nguvu yako mwenyewe kwenye hiyo projekti?

Vee Money: Kiukweli nimeanza na Jux, lakini kama kuna watu ambao wangependa kutusapoti, wanakaribishwa pia. Hapa niongeze kwa kusema kwamba watu wanaotuangalia nje wanafikiri sisi tunashirikiana kwenye muziki tu, hapana, tunafanya mambo mengi pamoja.

Over Ze Weekend: Unafanya vema kujihusisha na kazi ya jamii, una lolote la kuzungumza kuhusu watoto yatima?

Vee Money: Yah! Jamii itambue kwamba watoto yatima si kwamba wamependa kuwa vile, ni Mungu tu ndiye ameamua, tusiwaache peke yao, tuwafariji na kuwaonesha upendo.

Kwa upande wangu siku yangu ya kuzaliwa mwaka huu nili-kwe-nda kusher-ehekea na watoto ambao wana ugonjwa wa saratani pale Hospitali ya Muhimbili na kuwapa moyo na faraja pia ili waweze kujiona kwamba na wao wapo kwenye jamii na tunawapenda.

Kwa hiyo kila mmoja wetu katika nafasi yake anaweza kutoa mchango kwa jamii kwa namna yake.

Over Ze Weekend: Ni muda sasa upo kwenye uhusiano na Jux, ndoa lini?

Vee Money: Kiukweli naomba nisilizungumzie hili.

Over Ze Weekend: Wanamuziki kuwika mpaka wafanye kiki, je, nini mtazamo wako?

Vee Money: Ha!…Ha!…Haaa! Ndiyo nitapenda kulizungumzia. Kwangu, kikubwa ni kazi nzuri ambayo mashabiki wanakubali ndiyo ninaamini ni jambo kubwa kwa msanii kufanya, unaweza ukafanya kiki na kazi ikabuma.

Over Ze Weekend: Una kipi cha kuwaachia mashabiki zako?

Vee Money: Ninafanya kazi kwa bidii kwa ajili yao na nitahakikisha muziki unazidi kwenda mbele kuliko ulipo kwa sasa.

STORI:NEEMA ADRIAN

Comments are closed.