The House of Favourite Newspapers

Somalia yapiga marufuku Krismasi

0

Al-shabaab-131

Wapiganaji wa Kundi la Al Shabaab.

Serikali ya Somalia imepiga marufuku sherehe za kuadhimisha Sikukuu ya Krismasi katika mji mkuu wa Mogadishu.

Mkurugenzi mkuu katika wizara ya masuala ya dini, Sheikh Mohamed Khayrow, ameonya kuwa maadhimisho kama hayo yasiyofungamana na dini ya Kiislamu yanaweza kusababisha mashambulizi kutoka kundi la wanamgambo wa Al Shabab.

“Maofisa wote wa kulinda usalama wanapaswa kusimamisha ama kuvunja mikutano ya aina yoyote yenye nia ya kuadhimisha sikukuu hiyo isiyofungamana na dini ya Kiislamu.” alisema Sheikh Mohamed

Mwaka uliopita wapiganaji wa Al shabab walishambulia kambi ya majeshi ya muungano wa Afrika (AU) iliyopo Mogadishu wakati wanajeshi hao walikuwa wakisherehekea sikukuu ya Krismasi.

Wanajeshi 5 waliuawa katika shambulizi hilo la kuvizia.

Asilimia kubwa ya raia wa Somalia ni wasilamu.

Credit: BBC

Leave A Reply