The House of Favourite Newspapers

Spika Tulia Ampongeza Rais Samia kwa Kuongeza Mshahara wa Wafanyakazi

0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Akson akiongea wakati wa hafla ya uapisho wa wateule Ikulu, Jijini Dodoma

SPIKAwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza kiwango na kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma.

 

Dkt. Tulia amesema jambo hilo siyo dogo kwa ustawi wan chi hasa ukizingatia changamoto wananzozipitia wafanyakazi zote zinaelekezwa kwa wabunge kama wawakilishi wao na wao kama Bunge wanashukuru na kumpogeza sana Rais Samia.

 

Kwa upande mwingine Dkt. Tulia amempongeza Rais Samia kwa kitendo chake cha kuitangaza nchi kupitia filamu ya The Royal Tour kwani kwa kufanya hivyo amesaidia kutangaza utalii na ni jambo ambalo amelifanya kwa vitendo.

Hafla ya kuapisha wateule mbalimbali imefanyika leo Ikulu, Jijini Dodoma

Spika Dkt. Tulia amegusia pia ziara ya Rais Samia mkoani Tabora amabako alifanikiwa kuzindua barabara yenye urefu wa kilomita 342.9 inayotoka Tabora hadi Mpanda pamoja na barabara nyingine iliyopo ndani ya Mkoa wa Tabora, akibainisha kuwa hatua hiyo ni muhimu sana kwa maendeleo ya Mkoa lakini kwa ukuaji na ustawi wa uchumi nchi nzima.

 

Spika wa Bunge Dkt. Tulia ameyasema hayo wakati alipopewa nafasi ya kuongea wakati wa hafla ya uapisho wa wateule mbalimbali katika nafasi za Wenyeviti wa Bodi na Watendaji wa Taasisi mbalimbali, hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

Leave A Reply