The House of Favourite Newspapers

SPOTI XTRA ALHAMISI LAANZA KWA KISHINDO – PICHAZ

Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally, akimuuzia mteja Gazeti la Spoti Xtra kwenye foleni ya Mataa ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

HAYAWIHAYAWI hatimaye yamekuwa, baada ya maombi ya muda mrefu ya wasomaji wetu, Gazeti Bora la Michezo nchini, Gazeti la Spoti Xtra leo Alhamisi, Septemba 20, 2018 limeanza kutoka mtaani mara mbili kwa wiki, yaani kila Alhamisi na Jumapili.

…Akipokea pesa baada ya kumuuzia Gazeti la Spoti Xtra mteja huyo.

Wafanyakazi wa Global Publishers wakiongozwa na Mhariri Mtendaji, Saleh Ally,  wametinga mtaani katika maeneo ya Ubungo, Mawasiliano, Makumbusho na sehemu nyingine za Jiji la Dar es Salaam kuuza Gazeti la Spoti Xtra sambamba na kuwaelimisha ubora wa gazeti hilo na vitu vilivyomo ndani yake.

Mmoja wa Mavenda akimuuzia mteja Gazeti la Spoti Xtra kwenye foleni ya Mataa ya Ubungo.

Spoti Xtra limesheheni takwimu za soka na michezo mbalimbali inayopendwa duniani, uchambuzi makini wa mechi na masuala ya michezo bila kusahau ratiba na matokeo ya ligi zote kubwa duniani.

Saleh akilininadi Gazeti la Spoti Xtra kwa mteja, maeneo ya Ubungo.

Aidha, Spoti Xtra limesheheni makala za kuvutia za michezo, stori za burudani na mastaa wa ndani na nje ya nchi.

…Akichukua Gazeti la Spoti Xtra kutoka kwa venda.

Unaambiwa kwamba, Spoti Xtra linakupa uhondo zaidi kwa #Jero, pia linakupa fursa ya kushinda zawadi kibao zikiwemo jezi orijino za timu za Ulaya uzipendazo.

Venda akiwauzia Gazeti la Spoti Xtra abiria waliokuwa kwenye daladala leo asubuhi maeneo ya Ubungo – Mataa.

Wapenzi wa michezo wamestuka, hawaendi kwingine, bali ni Spoti Xtra pekee, mwambie na mwenzako, #SpotiXtra ndo’ habari ya mjini.

Saleh na venda wakimshawishi dereva wa daladala kununua Spoti Xtra.

Ndani yake kuna kuponi itakayokupa nafasi ya kushinda zawadi kibao, hujachelewa  #SpotiXtra #HapaNiUhondoTu kila Alhamisi na Jumapili.

…Akijitayarisha akimpa zawadi ya tisheti na kofia mteja wa Spoti Xtra ambaye pia alikuwa abiria kwenye daladala hiyo.

 

Zawadi ikitolewa.

 

Mwandishi wa Spoti Xtra, Omary Mdose (katikati) akiwa na mavenda wakati walipokuwa wakiuza gazeti hilo.

 

Mhariri Msaidizi wa Spoti Xtra, Samson Mfalila, akimuuzia Gazeti la Spoti Xtra abiria wa daladala.

 

PICHA NA SWEETBERT LUKONGE | GLOBAL PUBLISHERS

Kishindo cha Gazeti la Sport Xtra Chatikisa Jiji

Comments are closed.