The House of Favourite Newspapers

Steve Nyerere Ashusha Mijengo 3 Kwa Mkupuo!

MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amedhihirisha kwamba fedha inaongea baada ya kushusha mijengo mitatu kwa mkupuo.

 

Muigizaji huyo anaporomosha mijengo hiyo maeneo ya Nakasangwe Tegeta jijini Dar ambapo hivi karibuni, Amani lilifika na kukuta ujenzi unaendelea.

 

“Yupo vizuri, kipindi kama hiki kujenga nyumba tatu kwa mpigo siyo kitu kidogo, ana mtonyo wa kutosha,” alisema mmoja wa wajumbe wa eneo hilo ambaye aliomba hifadhi ya jina.

 

Alipotafutwa Steve Nyerere kupewa pongezi hizo alishukuru na kusema yeye siyo mtu wa kuanika sana mambo yake binafsi hivyo hawezi kuzungumzia gharama alizotumia kwenye ujenzi.

Stori: Memorise Richard

Comments are closed.