The House of Favourite Newspapers

STEVE NYERERE: MZEE MAJUTO ATATIBIWA INDIA – VIDEO

Mwenyekiti wa Wasanii, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’, akimjulia hali Mzee Majuto aliyelazwa katika Hospitali ya Tumaini Jijini Dar es Salaam.
..Steven Mengele ‘Steve Nyerere (kushoto) akiendelea kuzungumza na Mzee Majuto.

WASANII wa Bongo Muvi leo wamemtembela Muigizaji Mkongwe Nchini, King Majuto, ambaye amelazwa katika Hospitali ya Tumaini iliyopo Upanga Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kumjulia hali hospitalini hapo, Mwenyekiti wa Wasanii, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’, amesema kutakuwa hakuna haja ya wasanii hao kutoa michango mikubwa mara tu, mzee Majuto atakapopoteza maisha, kwahiyo wamejipanga na kumtafutia tiketi mbili ili aweze kwenda India kupata matibabu.

NA DENIS MTIMA/GPL

 

Comments are closed.