The House of Favourite Newspapers

Takukuru Yampandisha Kortini Aliyekuwa Kamishna Mkuu TRA

1

Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya (katikati) sambamba na waliokuwa wafanyakazi wa Benki ya StanBic Tanzania, Sioi Sumari (kushoto) na Bi. Shose Sinare (kulia), wakiwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam leo, wakisubiri kusomewa mashtaka yanayowakabili. 1v

TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini, TAKUKURU leo imewapandisha kortini aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA Harry Kitilya, Bi. Shose Sinare na Siyoi Abraham Solomon.

Takukuru imewafikisha vigogo hao katika  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kushtakiwa kwa makosa nane, ikiwemo tuhuma za kujipatia fedha kiasi cha Dola za Marekani milioni 6, mwezi Machi mwaka 2013, ili kufanikisha mkopo kutoka Benki ya Stanbic kwenda serikalini. Watuhumiwa hao wamekana makosa na kurudishwa rumande hadi April 8, 2016

 

Comments are closed.