The House of Favourite Newspapers

Taliban Wapiga Marufuku Unyoaji wa Ndevu Afghanistan

0

WAPIGANAJI wa Taliban wamepiga marufuku , vinyozi katika mkoa wa Helmand nchini humo kutowanyoa au kuwapunguza ndevu wanaume, wakisema hatua hiyo inakiuka sheria ya Kiislamu,‘’Mtu yoyote anayekiuka sheria hiyo ataadhibiwa’’ , Askari wa Taliban wamesema.

 

Baadhi ya vinyozi katika mji wa Kabul wamesema kwamba pia wao walipata maagizo kama hayo, maagizo hayo yanasema kuhusu kurudishwa kwa sheria kali kama zile zilizokuwepo wakati kundi hilo lilipokuwa madarakani awali , licha ya ahadi ya kwamba litaanzisha serikali itakayokuwa na misimamo ya wastani.

Tangu ilipochukua madaraka mwezi uliopita, Talibani imewapatia adhabu kali wapinzani wake, siku ya Jumamosi , wapiganaji wa kundi hilo, waliwapiga risasi na kuwaua watekaji wanne na miili yao kuzungunshwa katika barabara ya mkoa wa Herat.

Katika ilani iliochapishwa katika saluni, kusini mwa mkoa wa Helmand , maafisa wa Taliban walionya kwamba vinyozi lazima wafuate sheria ya Kiislamu katika kunyoa nywele za kichwani na ndevu.

Leave A Reply