The House of Favourite Newspapers

Ruth Mlay Kuweka Historia Dar Kesho…Kuzindua Albam

WAIMBAJI wengi wa muziki wa Injili Bongo, wanatarajia kufurika kwenye uzinduzi wa albam ya mwanamuziki mwenzao, Ruth Mlay inayotarajia kufanyika kesho Desemba 8, 2019 mwaka huu katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Changanyikeni jijini Dar.

Kwa mujibu wa waandaji wa shughuli hiyo ya uzinduzi, kutakuwa na waimbaji wengi wa nyimbo za Injili watakaopewa nafasi ya kuimba nyimbo zao kabla ya kuizindua rasmi albam hiyo kuanzia saa nane mchana. “Albamu inakwenda kwa jina la Sikuachi Bwana, ni albamu nzuri ambayo imesheheni nyimbo zenye ujumbe mzuri wa kumsifu na kumtangaza Kristo,” alisema Ruth.

Waimbaji watakaoupamba uzinduzi huo siku hiyo ni pamoja na Upendo Mtaita, Natasha Lisimo, Mwana wa Mfalme, Essau Eldad, Anna Luboya, Charles Yohana, Joshua Mbona na Steven.

Wengine ni Jesca Gazuko, Sarafina Shamdima, Elynes, Kelvin Audax, Aniset Butati, Subira na Dk Tumaini.

 

Comments are closed.