The House of Favourite Newspapers

Tatizo la nguvu za kiume, maana yake na tiba

0

Tumekuwa tukitoa elimu muhimu juu ya afya zetu kupitia makala mbalimbali katika ukurasa huu, leo ningependa nianzishe mada muhimu na yenye mguso mkubwa kwa jamii ya wanaume wa karne hii ya sasa.

Tatizo la nguvu za kiume limekuwa likiwasumbua wanaume wengi na limekuwa ni chachu ya kuvunjia kwa ndoa nyingi. Japokuwa tatizo hili linatibika na mtu akareje katika hali yake ya kawaida, wanaume wengi wamekuwa wakiona aibu kufika katika vituo vya tiba au kuonana na matatibu ili kupata ufumbuzi wa matatizo yao.

Neno nguvu za kiume ni neno linalomaanisha ‘uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’. Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine. Inaweza kuwa ni kujumuisha hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.

Kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi. Ni kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa au kuwahi kufika kileleni.

Hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka kutokana na umri. Kulingana na tafiti za kitabibu, wanaume wenye umri kuanzia miaka 60 tatizo hili ni kubwa kwao kuliko wanaume wenye umri wa miaka 40.

Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndiyo wanaokabiliwa sana na tatizo hili. Hii ni kwa sababu wanashindwa kuelewa aina ya chakula kinachoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, mtindo wa maisha wanayotakiwa kuishi ili kupunguza hatari hiyo, wanakunywa pombe na hawafanyi mazoezi ya viungo. Mazoezi ya mwili hupunguza hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume.

Usikose kufuatilia mada hii Alhamisi ijayo kwenye gazeti hilihili.

Leave A Reply