The House of Favourite Newspapers

TCAA YAIPA SIKU 28 FAST JEST, VINGINEVYO ITAIFUTIA LESENI

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imelipa notisi ya siku 28 Shirika la Ndege la FastJet Tanzania kabla haijalifutia leseni kwa madai kuwa shirika hilo halina hali nzuri ya kiuchumi na limepoteza sifa ya kuendelea na huduma hiyo.

 

Hayo yamesemwa leo na  Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari wakati akizungumza na wanahabari alipoeleza kwamba hadi kufikia Desemba 6, 2018, TCAA inaidai FastJet kiasi cha shilingi bilioni 1.413, ambazo ni tozo ya usalama na ya kuongozea ndege.

 

“Kwa mujibu wa sheria za anga, FastJet wamepoteza sifa ya uthibitisho, kwa sasa hawana ndege kwa sababu aliyewakodisha ametaka ndege yake isiruke na wameamua kuleta ndege mbadala yenye usajili wa nje lakini hiyo nayo imekuwa na matatizo.

 

“Mamlaka imezuia ndege hiyo (Fastjet) isiondoke hapa nchini kwa sababu shirika linadaiwa madeni mengi, TCAA pekee inadai zaidi ya bilioni 1.4. Kuruka angani huko ni hatari sana, sasa unapokuwa huna ‘accountable manager’ (mtaalamu wa masuala ya ndege) unakuwa huna sifa tena,” amesema Hamza.

 

Amesisitiza kwamba notisi hiyo inaanza leo Desemba 17, 2018 hadi Januari na  ametoa tahadhari kwa wananchi kutotumia usafiri wa shirika hilo ili kuepuka usumbufu na kwamba nia ya kusitisha huduma za usafiri na kulifuta kabisa huku likitakiwa kulipa fidia ya usumbufu kwa abiria.

 

“Tunaitaka FastJet ifuate masharti yetu kwanza kusitisha mauzo ya tiketi za abiria na waliopata madhara wafidiwe kwa mujibu wa sheria na pia wahakikishe wanalipa madeni yote,” alisema Hamza.

Mapema leo FastJet imetangaza kusitisha safari. Waliokata tiketi kurudishiwa fedha zao.

Comments are closed.