The House of Favourite Newspapers

TECNO CAMON X NA X PRO ZATAMBULISHWA RASMI

TECNO, kampuni ya simu za mkononi inayofanya vizuri barani Afrika inaendelea kutanua soko lake baada ya kuzindua simu mpya TECNO CAMON X yenye 20MP SELFIE, mfumo mpya wa Android 8.1 Oreo na Hios ya 3.3, ikiwa ni muendelezo wa toleo la ‘TECNO CAMON’ iliyozinduliwa nchini NIGERIA (LAGOSI), Tarehe 5/4/2018.

 

Kampuni ya simu ya TECNO hivi karibuni imeweza kuingia mkataba na moja kati ya kampuni bora katika upande wa mitandao (GOOGLE) iliyozindua mfumo mpya ya uendeshaji wa simu za mkononi Android 8.0Oreo (Go edition), utakaotumika katika matoleo yote ya TECNO kwa ndani ya mwaka 2018.katika uzinduzi huo TECNO imejihakikishia uzalishaji na usambazaji wa simu zenye technolojia na ubora zaidi katika masoko zaidi ya 40 hasa katika nchi za Afrika.

 

Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi makamu wa raisi wa TRANSSION HOLDINGSambayo ni kampuni mama ya TECNO,Bwana Andy VAN alisema kwamba, “TECNO haizalishi simu kwa kuzingatia maoni ya wafanyakazi wetu tu, ila kampuni inazingatia zaidi ushauri na maoni ya watumiaji ili kuwapatia kilichobora zaidi ukilinganisha na zilizopita”.kupitia CAMON X yenye 20M SELFIE+16MP mtumiaji atakua na uhakika kupiga picha kwenye mwanga hafifu ya kupata picha inayovutia zaidi, CAMON X imeongezewa uwezo wa kung’arisha picha kwa asilimia 30% ya CAMON CX,

 

“Na katika kuhakikisha tunaenda na wakati TECNO imewaletea ‘FACE ID’ aina mpya ya (security) inayomuezesha mtumiaji kufungua simu kupitia paji la uso ambayo ni tofauti na alama za vidole (fingerprint) kama ilivyozoeleka”. Na kwa kuwapatia wepesi wa kufanya kazi kwa haraka zaidi CAMON X ina wigo mpana  wa kioo chenye nchi 6.0 na uwiano wa 18:9kinachompatia mtumiaji wepesi kugawa kioo na kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja. Alimaliza

 

CAMON X inampa mtumiaji uhuru wa kuperuzi na kuangalia video muda wowote pasipo na hofu ya kuishiwa chaji kwani uwezo wake wa betri ni 3750mAh iliyo na kasi ya mtandao wa 4G namemori ya 16GB ROM + 3GB RAM.

CAMON Xilitambulishwa pamoja CAMON X pro, ambayo ni tolea pacha kwa kudokezea baadhi ya sifa zake hasa upande wa kamera, ikiwa ni simu ya kwanza duniani kuwa na megapixel 24 mbele huku kamera yake ya nyumba ni sawa na ya CAMON CX yenye 16MP.CAMON X pro inauwezo mkubwa wa kuprosesi vitu kwa haraka zaidi ukilinganisha na toleo lolote la CAMON kwani prosesa yake ni 2.0ghz octa-core na memori ya 64GB ROM + 4GB RAM lakini simu iyo bado haijaingia sokoni rasmi.

Katika uzyaduzi  huo TECNO Tanzania, iliwakilishwa na  wasanii pamoja na waandishi wa habari kutoka vyomba mbalimbali vya Tanzania, msanii Rosary Iwole maarufu kama “ Rosa Ree” na wengineo walipata nafasi ya kushuhudia utambulishwaji wa simu hizi katika soko la dunia nchini Nigeria katika jiji la Lagos kwa mara ya kwanza.

TECNO Tanzania inatoa fursa kwa wateja wa awali wanaweza kutoa (pre order) kuanzia tarehe 13/4/2018.

 

Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya http//www.tecno-mobile.tz.com

Comments are closed.