The House of Favourite Newspapers

Tambwe Kurudi Simba

AMISSI TAMBWE-001

Hamis Tambwe

Na Mwandishi Wetu

WAKATI raundi ya pili ya Ligi Kuu Bara ikiwa imeanza na Simba kuonekana ikisuasua kwenye ufungaji, sasa habari kubwa klabuni hapo ni kutafuta dawa ya kuondoa tatizo la washambuliaji kushindwa kufunga mabao mengi na tayari jina la Amissi Tambwe limetajwa kikosini hapo.

Tambwe ambaye anaichezea Yanga, klabu ambayo ilimsajili akitokea Simba, amesikia taarifa hizo na akazitolea tamko pia.

Hali ya Tambwe kuonekana kuhitajika Simba ilijitokeza juzi kwenye mazoezi ya timu hiyo katika Uwanja wa Boko Veterani ambapo Meneja wa Simba, Mussa Mgosi ndiye ambaye alikuwa akipewa ujumbe wa kuhakikisha safu yao ya ushambuliaji inakuwa bora na kufunga kama ambavyo Tambwe amekuwa akifanya au alivyokuwa akifanya wakati alipokuwa kikosini hapo.

Tambwe & Busungu

…Tambwe akishangilia goli na wanachezaji wenzake mechi zilizopita.

Wakati Simba wakiendelea na mazoezi yao ya kawaida, kundi kubwa la mashabiki lilimfuata Mgosi aliyekuwa amekaa pembeni na kuanza kutoa malalamiko yao juu ya tatizo la ushambuliaji.

“Tuongee ukweli tu, Simba hatuna mshambuliaji aina ya Tambwe aliyekuwepo anaichezea Simba kabla ya viongozi wetu kumsitishia mkataba na kuondoka.Amissi-Tambwe

….Hamis Tambwe

“Angalia hivi sasa katika timu yetu tuna viungo wengi wachezeshaji wenye uwezo wa kutengeneza mabao kwa maana ya kupiga pasi za mwisho na krosi safi, lakini tatizo ni kwamba hatuna mshambuliaji anayesimama katikati anayevizia mipira kama Tambwe.

“Viongozi walimuacha Tambwe na kumsajili (Laudit) Mavugo, lakini chochote anachokifanya kama mashabiki tunaumia tukimuangalia mchezaji kama Tambwe akiendelea kufunga mabao,” alisikika mmoja wa mashabiki hao huku akiungwa mkono na wenzake.

Baada ya mashabiki hao kumzungumzia Tambwe na baadhi yao kuona kama kuna uwezekano arejeshwe kundini, Mgosi aliamua kuwajibu kwa kusema:

“Sidhani kama Simba tuna tatizo la ushambuliaji, sisi tatizo kubwa lililopo ni kuwa mashabiki ndiyo tatizo wanaosababisha washambuliaji wacheze kwa presha kubwa uwanjani.

“Mshambuliaji anapokosa bao anazomewa badala ya kupewa moyo wa kujituma ili akipata nafasi nyingine aitumie vema kwa kufunga, kiukweli siyo sahihi, ni vema mashabiki wakaliangalia hilo. tambwe

….Tambwe

“Tuna mastraika wengi wazuri kama Mavugo, Luizio (Juma), Ajib (Ibrahim) wote wana uwezo mkubwa wa kufunga.”

Alipotafutwa Tambwe kuzungumzia suala hilo na kama kuna uwezekano wa yeye kurejea Simba kwa kuwa mkataba wake unaelekea mwishoni, alisema:

“Mimi bado ni mchezaji halali wa Yanga, mkataba wangu utamalizika Juni, mwaka huu, nisingependa kuzungumzia hilo hivi sasa.

champs“(Anacheka kidogo) kiukweli nisingependa kulizungumzia hilo kwa hivi sasa, wao wanachotakiwa ni kutambua kuwa, mimi ni mchezaji halali wa Yanga.

“Wakati huohuo, wakati wa mazoezi ya Yanga, juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, kuna watu kadhaa walifika uwanjani hapo na kuanza kumrekodi kwa video Tambwe kitendo ambacho hakikumfurahisha kocha wake, George Lwandamina.

Baada ya mazoezi hayo kocha huyo aliagiza kutoruhusiwa kwa waandishi wa habari kuingia uwanjani kurekodi mazoezi yake kwa kuhisi wanaweza kuvujisha mbinu zake anazofundisha.

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.