The House of Favourite Newspapers

Times Fm Waja na Suka Suka, Ijumaa Kuvamia Mwembeyanga Dar!

suka4-001Mfano wa zawadi zitakazotolewa kwenye promosheni hiyo ya Suka Suka. suka2-001Walengwa wa promosheni hiyo ni wasusi.suka3-001Rasta aina ya Darling Hair zitakazotolewa kwa washindi.

KITUO cha Redio 100.5 Times Fm kinachorusha matangazo yake kutoka jijini Dar es Saalam ambao siku chache zilizopita waliwajaza wasikilizaji wao pesa za kutosha katika promosheni waliyoipa jina la ‘Dingilii Mapene’ sasa wanakuja na promosheni mpya inayoitwa Suka Suka.

Kupitia promosheni ya Dingilii Mapene, walikuwa wakitoa bidhaa mbalimbali kwa wasikilizaji wao. Walitoa unga, mchele, maharage pamoja na mapambo ya ndani zikiwemo kapeti pamoja na pazia.

Baada ya hapo walikuja na ishu ya kulipia wasikilizaji wake kodi za nyumba na wasikilizaji kibao walipata ‘dili’ hilo na kujikuta wakila kuku kwa mrija mwaka mzima baada ya kulipiwa kodi! Hii ndio times fm usioijua!

Sasa washikaji kwa sasa waja na kali zaidi ya hizo, wajua ni kitu gani?

Soma hapa….

Jamaa hawa baada ya kugundua kuna mambo mengi ambayo wasikilizaji wao wanahitaji. Wameamua vyovyote vile kuingia mtaani na kusaka wote wenye uwezo wa kusuka na kuwawezesha!

Times Fm kituo ambacho kinajipambanua kama ni moja kati ya Redio zilizoamua kwa dhati kuurudisha Uafrika nyumbani kwa slogani yao ya ‘Kiafrika Zaidi’ sasa wameamua kuingia ‘kitaani’ kusaka akina dada na kaka wenye uwezo mkubwa na kuwawezesha kwa lengo la vijana hao kufikia malengo yao kupitia vipaji vyao ambapo wenyewe Times Fm wanaita #SUKASUKANATIMESFM.

Akizungumza na Global Digital, mratibu wa SUKA SUKA NA MAKAVU LIVE, Namiundu Ngutupari ‘Jeshi’, amesema lengo la promosheni hizo ambazo zimekuwa zikisimamiwa na mtangazaji mahiri wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani Khadija Shahibu ‘Dida’, ni muendelezo wa Times Fm katika kurudisha fadhila kwa wananchi na kuwasaidia katika kufikia malengo yao waliojiwekea.

“Unajua Times Fm si Redio yetu ni Redio ya watanzania na ndio maana kwa muda mrefu tumekuwa tukifanya kila linalowezekana kurudisha fadhila kwa wasikilizaji wetu.”

Alisema kwa sasa watapita kila kona ya mkoa wa Pwani na Dar es Salaam katika kuitangaza Suka Suka na Makavu Live kwa lengo la kuwaambia vijana kuna nafasi wanaweza kuzitumia kupitia vipaji vyao.

Jeshi alibainisha kuwa kwa sasa wanajiandaa ambapo Ijumaa ya wiki hii  watakuwa maeneo ya Mwembe Yanga, jijini Dar es Saalam  ambapo watatoa zawadi mbalimbali zikiwemo nywele bandia (Rasta)aina ya Darling Hair, T- Shirt pamoja na burudani kabambe toka kwa wasanii mbalimbali.

 

Comments are closed.