TUNDA: SIONI TATIZO KUMPOST CASTO !

Anna Kimaro ‘Tunda’

BAADA ya penzi lao kuvunjika na kila mtu kushika hamsini zake, kwa mara ya kwanza mrembo anayenogesha video za wasanii Bongo, Anna Kimaro ‘Tunda’ amemposti mpenzi wake wa zamani ambaye pia ni Mtangazaji wa Clouds TV, Casto Dickson na kusindikiza na maneno ya kumtakia heri katika siku yake ya kuzaliwa.  

 

Katika ukurasa huo Tunda aliandika hivi; “Happy birthday mzee vizuri @ Castodickson ishiiiii” maneno yaliyozua gumzo mtandaoni na kuwafanya watu wajiulize kama wameamua kurudiana au la ndipo Tunda akafunguka:

“Mnajua nyie mnachekesha sana, sasa kwani kuna tatizo gani mimi kumposti huyo kaka, kwa sababu binafsi sioni kama ni tatizo kwa kuwa kila mtu alishaamua kushika hamsini zake, hakuna mapenzi tena sasa hivi tumebaki washikaji tu naomba mnielewe.” Hata hivyo, picha hiyo hakuiacha muda mrefu akaifuta kwenye akaunti yake.

STORI: MEMORISE

Loading...

Toa comment