The House of Favourite Newspapers

TUSUA MAISHA NA GLOBAL: Washindi Droo ya Tatu Waanikwa – Video

KAMA kawaida kila Jumanne ya wiki, droo ya tatu ya Shindano la Tusua Maisha na Global imefanyika tena leo Julai 10, 2018 ambapo washindi wanne wamepatikana na kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo Pikipiki mpya, set ya vyombo vya ndani (dinner set), Headphone na Jezi orijino ya timu ya Taifa ya Uingereza.

 

Droo nyingine inatarajiwa kuchezeshwa wiki ijayo Jumanne, ili kushiriki na kuibuka mshindi ni rahisi sana, nunua magazeti yanayochapishwa na Global Publishers ambayo ni, Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi Mchanganyiko, Amani, Ijumaa, Risasi Jumamosi, Spoti Xtra na Championi, utakuta kuponi ukurasa wa pili, ijaze na kisha ufuate maelekezo ili uweze kutusua maisha na Global na mwisho wa siku uibuke mshindi.

Comments are closed.