The House of Favourite Newspapers

Tyga Atakiwa Kurudisha Bil 1.5 Alizotapeli Dubai

Tyga.

MWANAMUZIKI wa Marekani, Tyga,  anadaiwa aarudishe fedha aliyopewa na gharama za tiketi alizokatiwa yeye na kundi lake kwa ajili ya kufanya shoo nchini Dubai kwa vile hakutokea.

Tyga alikuwa anatakiwa kutumbuiza sehemu mbalimbali katika Falme za Kiarabu mwezi Aprili mwaka huu na akawa amepewa fedha ya mwanzo ambazo ni $120k  na $21k za tiketi, hivyo anadaiwa kurejesha jumla ya $141k ambazo ni sawa na Sh. mil.  320.

Zaidi ya hapo anadaiwa kulipa $600k (Sh. bil. 1.3) kwa ajili ya hasara iliyopatikana kwa ajili ya matayarisho ya shoo hizo.

Pamoja na hayo, Tyga amekiri madai hayo na ameahidi kulipa.

Comments are closed.