The House of Favourite Newspapers

Tyga: Nilionywa Kutompenda Kylie, Nikapotezea

 

kylie-jenner-tyga-2968c941-1fd1-4e36-a132-985853aca6f5

Michael Ray Stevenson ‘Tyga’ na Kylie Jenner.

Mwanamuziki Michael Ray Stevenson ‘Tyga’, amefunguka kuwa amewahi kuonywa kutoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na Mwanamitindo Kylie Jenner lakini cha ajabu hakuambiwa sababu za kuwa mbali na mwanamke huyo hivyo akapotezea.

Akizungumza na Jarida la Complex, Tyga alisema yeye alikuwa na mapenzi ya dhati na mwanamke huyo lakini kila alipokutana na marafiki zake walimtahadharisha kuwa mbali naye.

attends the 2015 MTV Video Music Awards at Microsoft Theater on August 30, 2015 in Los Angeles, California.

“Marafiki zangu wengi walikuwa wakinitahadharisha kuwa mbali na Kylie bila kunipa sababu, nilishindwa kuwasikiliza kwani moyoni nilimpenda sana,” alisema Tyga.

Comments are closed.