Uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu mauaji ya MKIRU (Mkuranga, Kibiti, Rufiji)
Kabla ya kuingia kwa kina kwenye uchambuzi huu, ni muhimu kueleza bayana kwamba japo maana, mbinu na ufanisi wa uchambuzi wa kiintelijensia (‘intelligence analysis’ kwa kimombo) kati ya mie niliyepo hapa Glasgow na afisa mchambuzi wa intelijensia aliyepo Dar zaweza kuwa karibu na sawa, mazingira kati yangu na ya afisa huyo ni tofauti. Tofauti sio kwa vile mie nipo Uingereza na afisa husika yupo Tanzania bali vitu kama shinikizo la kupata majibu upesi na nyenzo mbalimbali kama vile watoa habari, mafaili, nk.
Pili, nitajitahidi kadri nitakavyoweza kuepuka ‘mtazamo wangu’ na badala yake niongozwe na kanuni za uchambuzi wa kiintelijensia. Hata hivyo, ni muhimu kufahamu kuwa moja ya nyenzo muhimu kwenye intelijensia ni mwanadamu, iwe kwenye kukusanya taarifa za kiintelijensia, kuchambua au kushauri. Kwahiyo, japo nitajitahidi kuepuka ‘mtazamo wangu,’ siwezi kuepuka ubinadamu wangu kama mchambuzi wa kiintelijensia wa somo husika.
Kwa kifupi, tuanze na tunachofahamu hadi muda huu. Kwa mujibu wa taarifa zilizopo mauaji yanayojumuisha eneo la Mkuranga, Kibiti na Rufiji (MKIRU) yalianza Januari 2015 na hadi sasa yamegharimu uhai wa watu 40 wakiwemo askari polisi 13.
Tukisema tuorodheshe mlolongo wa kauli za viongozi mbalimbali, wa serikali na wa jeshi la polisi, basi huenda itabidi kukesha hapa, au kuandika kitabu kizima. Hata hivyo, kwa kifupi, miongoni mwa kauli hizo ni kama ifuatavyo
Rais John Magufuli:
Kwa ujumla, Rais Magufuli ametoa matamko makubwa matatu kuhusu mauaji yanayoendelea katika eneo la MKIRU. Tamko la kwanza ni salamu za rambirambi alizotoa kufuatia mauaji ya askari polisi wanane, ambapo alilaani mauaji hayo. Hiyo ilikuwa April 14 mwaka huu.
Tamko la pili la Rais lilikuwa majuzi alipofanya ziara mkoani Pwani ambapo Juni 20 aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa serikali na vyombo vya dola ili kukomesha mauaji hayo. Rais alieleza kuwa watu wanaofanya vitendo hivyo vya mauaji “tunakaa nao, tunawaficha, ni watoto wetu.” Kadhalika, Rais Magufuli alieleza kuwa “serikali ya Awamu ya Tano sio ya kuchezewa” na kudai kuwa “(wauaji hao) wameshaanza kunyooka.”
Hata hivyo, siku moja baada ya Rais kutoa kauli hiyo ya kutia matumaini, askari polisi wawili waliuawa na gari lao kuchomwa moto, pengine ikiwa ni jibu la wauaji hao kwa Rais aliyedai kuwa “wameshaanza kunyooka.”
Tamko la tatu la Rais, na pengine kali kuliko hayo mawili, lilitolewa jana jijini Dar wakati wa uzinduzi wa upanuzi wa Bandari ya Dar, ambapo katika kilichoonekana bayana kuwa majibu kwa rai ya Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kwa Rais Magufuli kumtaka atafakari kuhusu ‘mashehe wa Uamsho’ wanaosota gerezani kwa miaka minne sasa bila kesi yao kuamuliwa.
Katika tamko hilo Rais aliwaomba wanasiasa wanaosema kuwa hawa (mashehe wa Uamsho) wameshikiliwa kwa muda mrefu “wajizuwie midomo yao,” na kudai kuwa “hata kuna watu kule Marekani walikaa Guantanamo muda mrefu,” na kudai kuwa (wanaoongea kama Lowassa kuwa kesi yao ishughulikiwe) inaweza kuwafanya watu kuhisi (anayesema hivyo) ni “mmoja wao.”
Rais Magufuli alihoji “kwanini hata siku moja mtu asijitokeze kualaani wanaouawa bila hatia kule (MKIRU), lakini kwa kutafuta sifa za kisiasa, mtu anatoka anasema watu wako ndani muda mrefu.” Rais aliwataka polisi kufanya kazi yao, na kuwaagiza kuwakamata “hao wanaoropoka waisaidie polisi,” na “msiogopee sura, awe na mwendo wa haraka, polepole au kukimbia, mkamateni kusudi akaisaidie polisi kule ndani.”
Rais alidai pia mtu aliyekamatwa na sare 500 za jeshi zilizokamatwa hivi karibuni “inaonekana anahusiana na walioko ndani (mashehe wa Uamsho).”
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba na Naibu Waziri wake Yusuph Masauni
CCM tu? Hako kamchezo tumeshakagundua. Dhahiri, huo ni ushamba wa vyama vingi.”
kuharakisha zoezi hili ambalo kwa hakika kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu kwa sisi
tunaosimamia haki na uhai wa raia wasio kuwa na hatia hii vita lazima tushinde
inshaallah,” alinukuliwa Masauni hivi karibuni.
Rais anakosea Sana kuhusisha suala la Masheikh waliopo ndani na mauaji ya MKIRU. Amewapa maadui silaha. Acha… https://t.co/wKq2QY6SN2— Zitto Kabwe Ruyagwa (@zittokabwe) July 2, 2017
Tunawatangazia
wananchi tumewaua hawa kwa sababu wanadhulumu watu kwa kutumia kazi zao na
yeyote atakayefanya kazi hapa au nje ya hapa tutamtafuta hadi nyumbani kwake.
Sisi tumejitolea kufa kuliko kuishi, kwa hiyo
dereva au raia popote uwaonapo toa taarifa iwe nyumbani au kazini.
Hakuna
njia ya kumaliza dhuluma isipokuwa chuma tu, hapa chuma tuuu!
Jumla ya kura zilizopigwa ni 496, na matokeo ndio hayo pichani. #TanzaPoll inawashukuru nyote mlioshiriki. Ripoti ya #MKIRU yaja hivi punde. pic.twitter.com/qugsa09SYZ— Evarist Chahali (@Chahali) 5 July 2017
Kama inavyoonekana katika ‘tweet’ hiyo yenye matokeo ya kura ya maoni, dhana kuu nne ni
- Ugaidi
- Chuki za kisiasa
- Chuki za wananchi dhidi ya Jeshi la Polisi
- Uhalifu kama mwingine
akiswalisha swala ya Isha, Ferouz Elias (27) na waumini wawili, Mbwana Rajab na Khamis Mponda.