The House of Favourite Newspapers

Uganda Yaagiza Dozi Mil. 2 Chanjo ya Covid-19

0

UGANDA  imeomba dozi zaidi ya milioni mbili za chanjo ya Covid 19, wakati idadi ya maambukizi ikiendelea kuongezeka katika taifa hilo na kufikia 25,000.

‘’Wizara imeomba chanjo hiyo ya AstraZeneca kupitia shirika la Global Vaccine Alliance (GAVI) na kuwa mchakato uko kwenye hatua za kuelekea mwishoni,” Ripoti ya tovuti moja binafsi imemnukuu Mkurugenzi wa huduma za afya, Henry Mwebesa, akiongea.

‘’Hii ni chanjo (AstraZeneca) ambayo serikali inatambua imepatiwa idhini na Shirila la Afya Duniani… ni muhimu kufahamu kwamba chanjo inayopitishwa na Wizara ya Afya na WHO ndiYo inaweza kupewa raia wa Uganda,’’ aliongeza.

Uganda inatarajiwa kupokea dozi milioni mbili kutoka Gavi mwanzoni mwa mwaka 2021 lakini “inatenga bajeti kwa ajili ya kunua dozi zaidi kwa ajili ya wananchi.’’

Kumekuwa na ongezeko la maambukizi kila siku wakati ambapo taifa hilo linajiandaa kwa uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 14 mwezi Januari 2021.

Baadhi ya wanasiasa wameshutumiwa kwa kukiuka masharti ya kudhibiti virusi vya Corona wakati wa kampeni.

Leave A Reply