The House of Favourite Newspapers

Uingereza: Mtanzania Aliyemuua Mkewe Ahukumiwa Jela Maisha

KEMA SALUM (39) Mtanzania aliyemwua mkewe Mtanzania pia, Lelya Mtumwa (35) kwa kumchoma visu nchini Uingereza , amehukumiwa na mahakama ya Old Bailey kwenda jela kwa miaka isiyopungua 23.

 

Mtu huyo ambaye alimchoma marehemu visu kikatili mara 49 mbele ya mwanaye wa kiume, alikiri mbele ya mahakama hiyo ambayo ilimhukumu kwenda jela maisha, lakini kwa taratibu za hukumu za Uingereza, iwapo mfungwa ataonyesha tabia njema, kifungo kitakuwa cha miaka hiyo 23.

 

Salum ambaye ana historia ya ukatili kwa mkewe mwingine waliyeachana naye, alikuwa akiishi Uingereza kwa visa ya miezi sita baada ya kumwoa Mtumwa nchini Tanzania.

 

Siku ya Machi 30 mwaka huu, alimchoma visu marehemu kwa madai ya wivu kwamba siku hiyo alikuwa ametoka kwenda matembezi na wanawake wengine ambapo kabla ya kumchoma visu alikuwa amejaribu kumnyonga nyumbani kwao eneo la Haringey, kaskazini mwa London.

 

Baada ya jaribio hilo alikimbilia jikoni na kuchukua kisu ambapo alimchoma marehemu na alipokamatwa alidai alifanya hivyo kwa kujihami. Mwanzoni mwa mashitaka Salum alikuwa amekana, lakini hatimaye alibadili na kukiri.

 

Imeelezwa akitoka jela atabandikwa muhuri kila mahali kuanzia kwenye kitambulisho chake mpaka mtandaoni kuwa ni muuaji na akiwa jela akawa mtovu wa nidhamu anaweza kuongezewa adhabu.

Yule Mtanzania Aliyeuawa Uingereza, Mume Akiri Alimuua!

Comments are closed.