The House of Favourite Newspapers

Ujue Undani wa Hamza, Aliyeua Askari kwa Risasi Askari-Video

0

JINA linalosomeka katika usajili wa simu yake ya mkononi alioufanya kwa alama za vidole, ni Hamza Hassan Mohammed na inaonesha kwamba alizaliwa Novemba 11, 1991.

 

Ni huyu ndiye aliyesababisha taharuki kubwa na umwagaji damu kwa askari watatu wa Jeshi la Polisi na mmoja wa Kampuni ya SGA huku wengine sita wakijeruhiwa.

 

Wakati bado tukio hilo lililotikisa kila kona ya nchi likiendelea kuwa gumzo kwenye vichwa vya wengi, Global TV imekuandalia wasifu mfupi wa Hamza, kulingana na jinsi watu mbalimbali walivyokuwa wanamjua, kabla hajatekeleza tukio hilo la kutisha, na huu ni undani wake.

 

Leave A Reply