The House of Favourite Newspapers

Umati Wafurika Shoo ya Bobi Wine Licha ya Manyanyaso ya Polisi

Image result for Bobi Wine Kyarenga concert

MAELFU ya watu walifurika katika ufukwe wa Kyarenga jana (Jumamosi) kushuhudia shoo iliyofanywa na mwanamuziki wa Uganda aliyejikita pia katika siasa, Bobi Wine, licha polisi kulipiga danadana onyesho hilo mara tatu wakiliahirisha.

Kwa mujibu wa mtandao wa  TUKO.co.ke, onyesho hilo lilikuwa lifanyike Uwanja wa Namboole, Oktoba 20, lakini polisi waliliahirisha kwa kumnyima kibali.

 

Hali hiyo ilimlazimu Bobi kuishutumu serikali ya Rais Museveni kwa kuendesha udhalimu dhidi ya wananchi wa Uganda akiwatumia polisi.

Comments are closed.