The House of Favourite Newspapers

Umoja wa Mataifa yazindua ripoti ya dawa za kulevya

0

2 Ofisa Mipango wa Umoja wa Mataifa, Immaculate Maliyamkono (kushoto) na Mfamasia Mkuu wa Kitengo cha Habari, Takwimu na Elimu, Amani Msami wakijiandaa kuzindua ripoti hiyo.1.Mfamasia Mkuu wa Kitengo cha Habari, Takwimu na Elimu, Amani Msami (wapili kutoka kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi huo.
3Wanahabari wakifuatilia hafla hiyo.

OFISI ya Habari ya Umoja wa Mataifa (UNIC) leo imezindua ripoti yake ya mwaka 2016 inayoelezea dawa za kulevya na athari zake katika Bara la Afrika.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam katika uzinduzi huo, Mfamasia Mkuu wa Kitengo cha Habari, Takwimu na Elimu, Amania Msami, amesema kuwa kumekuwepo na idadi kubwa ya ongezeko la biashara ya dawa za kulevya barani Afrika huku watumiaji wakiwa hasa ni vijana wadogo na kusababisha kuongezeka kwa vitendo viovu vinavyofanywa na magenge ya kihalifu.

Alisema ingawa kumekuwepo na jitihada zinazofanywa na nchi za Magharibi mwa Afrika kupitia Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (Economic Community of West Africa-ECOWAS) lakini bado takwimu zinaonesha idadi kubwa ikiongezeka kila kukicha.

Aidha Msami alisema Bara la Afrika limechukua hatua mbalimbali kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya, ambapo mwaka 2015 umoja wa Afrika uliandaa na kujadili mkakati wa kudhibiti dawa hizo hatari ili kuzuia kabisa mianya ya matumizi na kufanikiwa kuwatibu watumiaji wa dawa hizo.

Alisema ECOWAS iliandaa mpango kazi wa kupambana na biashara ya madawa ya kulevya na uhalifu wa kimataifa katika nchi za Afrika Magharibi zikiwemo Ghana, Misri na Nigeria, huku wakiitisha kikao na nchi ya Afrika Kusini kujadili njia bora ya kukabiliana na matumizi ya dawa hizo.

Vilevile alifafanua kuwa inakadiriwa katika Bara la Afrika kuna watumiaji nane wa bangi kati ya watu 100 wenye umri wa miaka kati ya 15 na 64 na watu watatu kati ya 100 wenye umri kama huo hutumia dawa za Heroin na Cocaine, idadi hiyo ikiwa ni kubwa kuliko wastani wa watumiaji wa dawa duniani.

(Na Denis Mtima/Gpl)

Leave A Reply