Una tatizo lolote kuhusu simu yako.. Tecno wamekujibu hapa

Kampuni inayoongoza kwa kuuza simu bora kwa gharama nafuu ambayo kila Mtanzania anaimudu, Tecno imefanya “kujiongeza” katika kukusaidia mteja wake kuhakikisha kwamba haupati tatizo lolote unapotumia simu zao na kupatiwa msaada wa haraka endapo utakuwa na tatizo.


 Timu ya Tecno imefanya mahojiano ya moja kwa moja na mashabiki wa mtandao wa kijamii wa Facebook maarufu kama “Facebook Live” ambapo ilijibu changamoto mbalimbali kutoka kwa watumiaji wa simu za Tecno. Akizungumza katika mahojiano hayo mtaalamu wa masuala ya ufundi kutoka Tecno John G.

 Ndazi alisema “Tumekuwa tukipokea baadhi ya maswali kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii kutoka kwa wateja wetu na bila shaka nyote mnafahamu kwamba hivi karibuni tumezindua simu mbili kali, kuna Phantom 6 na Phantom 6 Plus ambazo zimepokelewa vizuri na tukaamua kutumia Phantom 6 kujibu maswali kupitia Facebook Live ambapo tumejibu maswali kutoka kwa wateja wetu.” Pamoja nae alikuwepo Gilbert Asumwisye ambaye ni Mhandisi wa Programu.

Toa comment