The House of Favourite Newspapers

Undani wa Nisha Kumpora Bwana wa Wolper

HIVI unajua kuwa ubuyu nao una viwango vyake? Kuna ubuyu ambao ukiula unauchubua mdomo tu na kuna ule wa baba Issa ambao ukiula, unaishia kumeza mate kisha unatupa mbegu ikiwa tupu! Sasa taarifa ikufikie kuwa mwigizaji ambaye ni komediani mwenye jina kubwa Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’, anadaiwa kumbeba mzimamzima bwana wa staa mwenzake, Jacqueline Wolper Massawe, Barnaba Shelukindo ‘Brown’.

 

WALIANZA KITAMBO

Chanzo cha ubuyu huo kililifungukia Ijumaa Wikienda kuwa, Nisha na Brown walishaanza kunyemeleana kitambo tangu jamaa huyo akiwa mikononi mwa Wolper.

Ilisemekana kwamba, kufuatia uwepo wa mawasiliano ya siri kati ya Nisha na Brown, jamaa huyo alianza kuleteana vimbwanga vya kila kukicha na Wolper.

 

WOLPER AVUMILIA

Katika kipindi chote cha vituko, mara nyingi ilielezwa kwamba, Wolper alijitahidi kuvumilia kwa kuwa alihisi akimmwaga ghafla watu watasema kuwa hawezi kuwa na mwanaume kwa muda mrefu, lakini mambo yalipomzidia, uvumilivu ulimshinda mwanadashosti huyo.

“Huyu Nisha na Brown walianza mambo yao muda mrefu sana hata kabla ya jamaa huyo kuachana na Wolper.

“Sasa ninaona wameamua kuweka mambo hadharani,” alisema mtoa ubuyu ambaye ni mtu wa karibu kabisa wa Nisha aliyeomba hifadhi ya jina ili asitibue uhusiano wao.

‘Kikulacho’ huyo alizidi kumwaga ubuyu kuwa, Nisha na Brown kwa sasa wanapika na kupakua kwa raha zao.

 

 

Salma Jabu ‘Nisha’

 

 

HUYU HAPA WOLPER

Kabla ya yote, Ijumaa Wikienda lilimfikishia ubuyu Wolper ili kumsikia kama anajua kwamba Brown alinyakuliwa na Nisha ambapo mambo yalikuwa hivi;

Ijumaa Wikienda: Wolper hivi una habari kuwa Brown anatoka na Nisha?

Wolper: Jamani mimi sijui lolote, niko bize na cherehani yangu (kwa sasa anashona nguo) na mambo mengine hayanihusu kabisa.

Ijumaa Wikienda: Si ndiyo alikuwa baby wako?

 

Wolper: Sasa hivi sitoi kiki kwa mtu yoyote, niko bize na mambo yangu, mimi mambo ya watu siyajui kabisa.

Baada ya kumsikia Wolper na kumpa ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Brown na kumbananisha juu ya ishu hiyo ambapo mambo yalikuwa hivi;

Ijumaa Wikienda: Kuna habari kwamba sasa hivi umejiweka kwa Nisha baada ya kutoka kwa Wolper…je, imekuwaje?

Brown: Yaani hapa nilipo siwezi kuongea na simu kabisa…

 

Ijumaa Wikienda: Lakini mbona hapo unaongea?

Brown: Siwezi kabisa labda nikitoka hapa nilipo na sijajua nitatoka muda gani.

Ijumaa Wikienda: Ila tunamtafuta Nisha hapatikani, vipi uko naye hapo?

Brown: Yuko nje ya nchi, nitakupa namba yake ya huko aliko.

Hata hivyo, Brown hakutuma namba ya Nisha na huko nje aliko na alipotafutwa kwa namba yake inayofahamika, haikuwa hewani hivyo jitihada hizo zinaendelea.

 

NISHA APEWA ZA USO

Kufuatia madai hayo mazito, Nisha amekuwa akiwa za uso kwenye mitandao ya kijamii kutokana na matukio yake ya kupora mabwana wa wenzake tangu alipofanya hivyo Shilole kabla ya mwanadada huyo kuolewa na Uchebe mwishoni mwa mwaka jana.

Ubuyu: Imelda Mtema, Dar.

VILIO Vyatawala Familia ya Watu Sita Waliokufa Ajali ya Watu 26

Comments are closed.