The House of Favourite Newspapers

Ureno: Uwanja wa Ndege wa Madeira Wapewa Jina la Cristiano Ronaldo

STRAIKA wa Klabu ya Real Madrid Ronaldo na Timu ya Taifa ya Ureno, ambaye aliongoza taifa lake kushindwa ubingwa wa Ulaya mwaka jana, Christiano Ronaldo (32), alizaliwa katika Mji wa Madeira, Funchal na baadaye akachezea Sporting Lisbon na Manchester United.

Uwanja wa ndege wa Madeira ambapo alizaliwa fundi huyo wa soka, sasa umepewa jina la Cristiano Ronaldo.

Baadhi ya wanasiasa wa eneo hilo wamepinga uamuzi wa kubadilisha jina la uwanja wa Ndege wa Madeira kuwa Uwanja wa Ndege wa Cristiano Ronaldo.

“Wakati mwingine, shukrani za taifa huwa hazidumu sana, lakini Madeira haitasahau,” Miguel Albuquerque, rais wa serikali ya Madeira alitangaza, hatua ya kubadilisha jina la uwanja huo ilipotangazwa.

Comments are closed.