The House of Favourite Newspapers

Urusi Yaanza Awamu ya Pili ya Mapigano Nchini Ukraine Katika Jimbo la Donbas

0
          Majeshi ya Urusi yameanza kutekeleza awamu ya pili ya mapigano nchini Ukraine

MAPIGANO makali yametekelezwa katika miji ya Donbas ikiwa ni wiki kadhaa tangu Urusi iweze kusitisha mapigano yake katika nchi ya Ukraine.

 

Kwa sasa majeshi ya Urusi yamehamishia nguvu zake katika kushambulia majimbo yaliyopo Donestk na Luhansk pamoja na majimbo mengine yanaypatikana mashariki mwa nchi ya Ukraine.

 

Vyombo vya habari vya Ukraine vimeripoti kutokea kwa mashambilizi makali hasa katika miji ya Marinka,Slavyansk na Kramatorsk lakini pia vilithibitisha kutokea kwa mashambulizi makali katika Jiji la Kharkiv kaskazini mwa Ukraine, Mykolaiv Kusini na Zaporizhzhia kusini mashariki mwa Ukraine.

 

“Sasa tunaweza kuthibitisha kuwa Majeshi ya Urusi yameanza mashambulizi katika jimbo la Donbas amayo walikuwa wameyaandaa kwa muda mrefu, Majeshi mengi ya Urusi yameelekeza nguvu zao kwenye miji hiyo.” Alisema Zelensky katika hotuba yake ya kila siku kwa wananchi.

                                          Mashambulizi makali yanaendelea katika miji ya Donbas na Donetsk

“Haijalishi watakuja wanjeshi wangapi hapa kutoka urusi, tutapambana, tutalinda ardhi yetu, nawashukuru wapambanaji wote wanaoipigania nchi yetu hasa miji ya Donbas, Mariupol pamoja na miji ya Kharkiv ambayo tayari imeshikiliwa.”

 

Mashambulizi haya ya mara ya pili yanatazamiwa kama ndiyo yatakayotoa hatima ya pande zote mbili kwa maana ya Ukraine pamoja na Urusi.

                        Majeshi ya Ukraine yapo tayari kupambana na majeshi ya Urusi kulinda ardhi yao

Baada ya majeshi ya Urusi kurudi nyuma wiki mbili zilizopita kutokana na kushindwa kuukamata mji mkuu wa Ukraine Kyiv, ambapo majeshi hayo yalienda kujipanga kwa ajili ya mashambulizi ya awamu ya pili ambayo yamelenga kukamata miji ya mashariki mwa Ukraine.

 

Vikosi vingi vya Urusi vimeweka ngome katika mji wa Izyum ambao umezungukwa na mto Donetsk kiasi cha urefu wa maili 70 kutoka kusini mwa Kharkiv.

Leave A Reply