The House of Favourite Newspapers

Urusi Yamtimua Kazi Naibu Waziri wa Ulinzi, Ni Baada ya Kufeli Vitani

0
Naibu Waziri wa Ulinzi wa Urusi aliyetolewa madarakani Dmitry Bulgakov

NAIBU WAZIRI wa Ulinzi wa Urusi Dmitry Bulgakov ametimuliwa katika nafasi yake hiyo kufuatia madudu yaliyotokana na kushindwa kutimiza majukumu yake ya usambazaji wa vifaa na zana za kivita kitendo kilichosababisha majeshi ya Urusi kushambuliwa vikali na majeshi ya Ukraine.

Kanali Mikhail Mizintsev

Bulgakov ameondolewa na kuhamishiwa kwenye nafasi nyingine hiyo ni kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Ulinzi ya Moscow.

 

Nafasi yake inatarajiwa kuchukuliwa na Kanali Mikhail Mizintsev ambaye inaripotiwa kuwa ndiye aliyeongoza majeshi ya Urusi kuikamata Mariupol mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu.

Leave A Reply