The House of Favourite Newspapers

UTAIPENDA Zawadi Aliyojinunulia Whozu Baada Ya Mafanikio Yake.(PICHA & VIDEO)

 

Mchekeshaji na mwanamuziki chipukizi hapa Tanzania, Whozu amefanikiwa kutimiza ndoto yake ya kumiliki gari aina ya Mark X, hii ni baada ya kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye mikoa 13 kwenye tamasha la Togo Fiesta.

 

Msanii huyo ameonyesha furaha yake kwa kuwashukuru mashabiki kupitia akaunti yake ya instagram kwa kuweka post na gari aliyonunua ikiambatana na maneno yanayosomeka, “Niwashukuru pia Mshabiki zangu Asanteni sana kwa support Mwenyezi Mungu Awabariki sana.Shukrani pia Kwa Media Zote Nawashukuru kwa Nafasi yangu Kwenu🙏 Shukrani pia kwa Producers @osam_lucifer Hakika najua unafuraha Uliniamini Nami nikakuaminisha. Pia Zombie Langu @s2kizzy haha Nilikwambia Lakini! Asante pia Directors @lucca_swahili & @joowzeytz May God bless you all Fam & Fans🙏🙏 #GODISGOOD”

 

Aliendelea kutoa shukrani zake kwa midia ambayo ilimfanikishia mpaka yeye kufikia hapo alipo, “Wengi walikuwa wananitizama kama mchekeshaji lakini clouds wakanitizama kama entertainer…wakanifungulia dunia nakunipa Nafasi ya mimi kujifungulia maisha…. Kuperfom Fiesta 13 kati ya Fiesta 15 Mungu ni mwema
#mynewride mpiraaa mpyaaaa napiga round nazunguka dar nzima nikimaliza naunganisha kwenda moshi..
MUSIC PAYS #MatundaYaTigofiesta”

 

Kwa mwaka 2018, Whozu amefanya vizuri kwenye muziki na ngoma yake ya Huendi kwa Mbinguni, na ndio wimbo uliomfanya atumbuize karibia mikoa yote iliyopitiwa na Fiesta.

 

Piiiii piiiiiii piiiiiiii DINGOOO NA GARI YAKEEEEEE #Somaaaaaaaaiyooooooo

17.1k Likes, 668 Comments – Dingoo (@whozu_) on Instagram: “Piiiii piiiiiii piiiiiiii DINGOOO NA GARI YAKEEEEEE #Somaaaaaaaaiyooooooo”

Comments are closed.