The House of Favourite Newspapers

Utawala wa Kijeshi Wakaidi Wito wa ECOWAS

0

WATAWALA wa kijeshi nchini Guinea jana wameondoa uwezekano wa kumruhusu rais wa zamani anaeshikiliwa Alpha Conde kwenda uhamishoni, na kusema mchakato wa mpito kuelekea utawala wa raia utafanyika kulingana na matakwa ya raia wa nchi hiyo.

 

Taarifa ya baraza la uongozi huo, imetolewa katika kukaidi shinikizo la kimataifa la kuachiwa huru Conde na kuwasilisha ratiba ya miezi sita ya kuandaliwa kwa uchaguzi, baada ya mapinduzi ya Septemba 5 kuibua ukosoaji wa kimataifa.

 

Katika mkutano wa kwanza wa baraza hilo la uongozi na wanahabari kuhusu muda wa mwisho wa miezi sita wa kuandaliwa kwa uchaguzi.

 

Msemaji wake kanali Amara Camara amesema kuwa kiongozi wa mapinduzi hayo Mamady Doumbouya ameuambia ujumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS unaozuru nchini humo kwamba ni muhimu kwa Jumuiya hiyo kusikiliza matarajio halali ya watu wa Guinea na kwamba ipo haja ya kutorudia makosa ya zamani.

 

Leave A Reply