The House of Favourite Newspapers

Utokwaji na Majimaji Katika Via vya Uzazi vya Wanawake

0

Na MWANDISHI WETU/GPL

KWA kawaida wanawake hutokwa na ute katika via vya uzazi na hasa wale waliopevuka na kuwa na uwezo wa kuzaa. Hii ni njia moja wapo ya kutoa uchafu au  sumu mwilini. Hali hii ya ute kutoka huwa si ngeni na ni kawaida kabisa kwa wanawake wenye uwezo wa kuzaa.

Ute huu mara nyingi huwa hauna rangi ili kuutambua ni mpaka ukauke katika nguo za ndani. Ikumbukwe kuwa ute huu huwa ni kwa kiasi kidogo tu na hautoki mfululizo.

Leo ningependa msomaji wa makala haya  utambue majimaji ninayoyazungumzia yanaambatana na dalili mbalimbali kama vile:Kuwa na harufu mbaya. Kuna wakati mwanamke hutokwa na majimaji yenye harufu mbaya na harufu hii haitoki hata kama mwanamke huyo akioga na kubadili mavazi.

Pia harufu hiyo huwa kali zaidi pale mwanamke huyo anaposhiriki tendo la ndoa na mwenzi wake kitu kinachofanya asifurahie raha ya tendo la ndoa. Kuwashwa nje na ndani ya mlango wa via vya uzazi.

Hali hii kuna baadhi ya wanawake wanakumbana nayo sana na wanaona ni kawaida wanavumilia tu kumbe ni dalili ya hatari kwa afya ya uzazi. Maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa.

Ni wanawake wengi sana wanatokwa na majimaji machafu katika njia ya via vyao vya uzazi na wanaposhiriki tendo la ndoa na wenzi wao hupata maumivu makali sana kiasi ambacho wanashindwa kufurahia tendo la ndoa na wenzi wao lakini bado hawajui kama hilo ni tatizo.

Majimaji hayo huwa na rangi kama maziwa ya mtindi.

Kwa urahisi majimaji hayo huwa na rangi ya usaha, kumbuka ute wa kawaida unatambulika rangi yake mpaka ukauke kwenye nguo za ndani lakini ute huu unajibainisha waziwazi kwa kuwa na rangi hiyo ya usaha.

Maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo.

Kuna wanawake kila wanapohisi kwenda haja ndogo wanajuta kwani wanapata maumivu makali sana huku wakiona kuna majimaji huwa yanatoka katika via vya uzazi lakini bado hiyo hali haiwababaishi wanaendelea kuvumilia na kuona ni kawaida.

Via vya uzazi kubadilika rangi.

Mwanamke mwenye tatizo hili via vya uzazi hubadilika rangi na kuwa na rangi nyekundu kuliko rangi yake ya kawaida na wakati mwingine wekundu huo huambatana na michubuko, maumivu na vidonda. Mwanamke mwenye kutokwa na majimaji katika via vyake vya uzazi na kuziona dalili hizo ni wazi atambue kuwa hali hiyo si ya kawaida na ni vema akatambua kuwa atakuwa na maambukizi ya fangasi katika via vyake vya uzazi.

Na ni vema awahi kuwaona wataalamu wa afya ili afanyiwe vipimo na kupata matibabu mapema ili kuondokana na tatizo hilo. Unaweza kututafuta kwa ushauri na maswali.

Wiki ijayo tutaangalia nini chanzo cha wanawake wengi kukumbwa na tatizo la kutokwa na majimaji katika via vya uzazi au fangasi.

Leave A Reply