The House of Favourite Newspapers

Uwoya: Sitaki Kujitia Gundu, Maishani Mwangu nataka Furaha Tu

0
Irene Uwoya

IRENE Pancras Uwoya au Mama Krish; ni nembo ya tasnia ya Bongo Movies ambaye anasema kuwa, katika maisha yake hataki kujitia kero na gundu.

 

Uwoya anasema kuwa, kwa sasa mtu akijitia kero ni kujitakia mwenyewe kwa sababu kuna vitu vingi mno vya kumpa mtu furaha kila siku na siyo kero.

Irene Uwoya ndiyo Staa wa Bongo Movies mwenye mkwanja mrefu kwa sasa

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Uwoya anasema kuwa, alishasahau kero kitambo na ndiyo maana siku hizi anaachia nafsi yake kuwa na furaha tu na si kitu kingine.

 

Anasema hii ndiyo maana hivi karibuni aliamua kutafuta mtu wa kumchekesha ili roho yake ifurahi.

Uwoya amesema maishani mwake hataki gundu, anataka furaha tu

“Mimi sitaki kero wala kujitia gundu kwa kuwaza chochote kwenye maisha yangu haya hata siku moja.

 

“Hii ni kwa sababu sitaki kuyatia gundu maisha yangu hata kidogo, mimi nahitaji raha siyo karaha,” anasema Uwoya ambaye kwa sasa ndiye staa wa kike mwenye mkwanja mrefu Bongo nzima.

Cc; @sifaelpaul

 

Leave A Reply