The House of Favourite Newspapers

Uzinduzi wa Album Yake Mpya, Chin Bees Aisimamisha Dar – Video

MKALI wa muziki wa Trap, Chin Bees, anayetamba hivi sasa na ngoma yake ya ‘Kababaye’ amezindua labamu yake mpya inayoitwa LADHA, uzinduzi ambao umefanyika katika ukumbi wa Next Door, Masaki Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

 

Katika uzinduzi huo uliokuwa wa aina yake huku akiteka mashabiki jijini Dar, Chin Bees anayesimamiwa kazi zake za muziki na Kampuni ya Wanene Entertainment amesema kuwa Album hiyo itaanza kupatikana mtaani kuanzia leo Machi 3, 2018 na kila shabiki yake ataipata bure kama zawadi bila malipo yoyote.

MSIKIE MWWENYEWE AKIANIKA

Comments are closed.