The House of Favourite Newspapers

UZINDUZI WA GAZETI LA SPOTI XTRA ULIVYOBAMBA KITAA (Pichaz + Video)

Dereja Bajaj jijini Dar akisoma gazeti jipya la Spoti Xtra, pembeni yake ni muuzaji wa magazeti.
Msomaji mwingine akipewa maelekezo na muuzaji wa gazeti hili.
Wasomaji jijini Dar wakipewa ufafanuzi kutoka kwa muuzaji wa Gazeti la Spoti Xtra
Timu ya wauzaji wa Gazeti la Spoti Xtra wakiwa mtaani.
Msomaji wa Spoti Xtra akinunua gazeti hilo kutoka kwa muuzaji.

GAZETI jipya la michezo la Spoti Xtra ambalo ni gazeti dada na Gazeti la Championi linalotolewa na Kampuni ya Global Publishers, leo limezinduliwa rasmi kwa kutoa toleo lake la kwanza katika hafla iliyoendana na promosheni ya kuzunguka viunga mbalimbali vya Jiji la Dar es Salaam.

Katika promosheni hiyo, msafara wa wafanyakazi na wanenguaji waliokuwa wakisindikizwa na burudani ya muziki, ilianza mapema asubuhi katika ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam na kuelekea mitaa mingine ya Sinza, Mwenge, Ubungo, Mabibo, Manzese, Kinondoni, Mwananyamala, Makumbusho, Kawe, Tegeta na kumalizia Soko la Tegeta Nyuki ambapo wapenzi wa magazeti ya michezo walikuwa wamemaliza rundo la magazeti hayo yaliyokuwa yakiuzwa kwenye promosheni hiyo.

Gazeti hilo lililoonekana kubamba mitaani, wasomaji wa magazeti waliohojiwa na wafanyakazi wa Global waliokuwa kwenye msafara huo, hawakusita kuusifia mwonekano wa ndani na nje wa gazeti hilo.

Muuza magazeti kwenye Kituo cha Kawe, Dar aliyejitambulisha kwa jina la Juma, alionesha furaha yake waziwazi kwa kushangilia ujio wa Spoti Xtra lililosheheni habari za burudani, michezo na hadithi za kusisimua kutoka kwa watunzi mahiri na uchambuzi wa michezo.

Habari/Picha na Richard Bukos/GPL

Comments are closed.