The House of Favourite Newspapers

V Money Amaliza Bifu na Mdogo Wake

STAA wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘V Money’ amefunguka kuwa kwa sasa hana tena bifu na msanii mwenzake ambaye ni mdogo wake, Marianne Mdee ‘Mimi Mars’ kwa kuwa bifu hazina maana yoyote.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Vanessa alisema kuwa ameamua kumaliza tofauti kati yake na ndugu yake huyo kwa kuwa wao ni ndugu hivyo hakuna maana yoyote wao kutofautiana.

“Naona ni jambo jema kwa kuwa mimi na mdogo wangu tulikuwa hatupo pamoja kutokana na sababu tu ambazo hazina msingi. Kwa hiyo nimeona tumalize bifu letu na tuendelee kupeana sapoti katika kazi zetu japokuwa kila mmoja anafanya muziki wake,” alisema V Money.

 

NEEMA ADRIAN

EXCLUSIVE Alikiba: “Kutekwa kwa MO Dewji Nimeguswa Sana”

Comments are closed.