The House of Favourite Newspapers

Victory Campus Night, Kazi Ipo Dar – Ijumaa Hii!

 

VIWANJA vya Tanganyika Packers – Kawe, jijini Dar es Salaam,  patakuwa hapatoshi Ijumaa ijayo , Mei 17, 2019, kwani patakuwa na  tamasha la kimataifa na la kihistoria litakalofanyika kuwaunganisha wanafunzi wote wa vyuo vikuu nchini na nje ya nchi, watumishi wa Mungu na watu wote wenye kupenda kulijua neno la Mungu.

Victory Campus Night 2019, ambalo limeandaliwa na Kanisa la VCCT – Mbezi Beach, chini ya mchungaji Dkt. Huruma Nkone, hufanyika kila mwaka lakini mwaka huu kutakuwa na mambo mengi zaidi mazuri yatakayokuinua na kukufanya uwe wa tofauti.


Kutakuwa na maombi, kusifu, kuabudu, mafundisho mbalimbali ya neno la Mungu na nasaha kutoka kwa wahamasishaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi akiemo Eric Shigongo, zitakazokupa mbinu za kujikwamua.

Tayari mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili kutoka nchini Zimbabwe, Mkhuhuli Bhebhe, anayetamba na wimbo ujulikanao kama Ndiyeyu Jesu Medley, ameingia nchini Tanzania jana na ndiye atakayeongoza jahazi la burudani kwenye tamasha hilo.

Mbali na Mchungaji, Dr. Huruma Nkone na Eric Shigongo, wengine watakaounguruma jukwaani hapo ni pamoja na mtangazaji wa Clouds Media, Samuel Sasali.

Pia watakuwepo wasanii kibao kutoka kiwanda cha nyimbo za Injili hapa nchini akiwemo Masanja Mkandamizaji, Upendo Nkone, Dr. Ipyana Kibona, Joel  Lwaga, TCG Dance, Winners of Students Audition na wengine wengi.

VICTORY CAMPUS NIGHT; Moto Wa Kuotea Mbali; Mkhululi Bhebhe, Ahusika…

Comments are closed.