The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Hii Ndiyo Safari ya Muziki ya Producer King Lufa Aliyetengeneza ‘Bilima’ ya Nuh Mziwanda

UMEWAHI kuinyaka hii mtu wangu wa dhahabu? Kama wewe ni mfuatiliaji wa tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, lazima utakuwa umeshawahi kulikisia jina la Producer King Rufa.

Global TV Online imepiga stori na Producer King Rufa ambaye alizaliwa na kukulia Arusha kisha kuibukia Dar katika harakati za kusaka maisha na mkwanja kwa ujumla.

Rufa ameanika maisha halisi aliyoanza nayo wakati anajifunza u-producer akieleza kuwa alianzia gheto mkoani Arusha akiwa na laptop yake na speakers za kawaida bila monitor speakers, hapo ndipo alianza kutengeneza bits mwenyewe wakati alipotoka shule.

Baadaye ndipo aliamua kukimbilia Dar ili kufanya mchakato wa kukuza zaidi kipaji chake ili afikie ndoto zake. Pamoja na hayo alifanikiwa kukutana na msanii Quick Rocka ambaye naye ni producer mkali tu Bongo, hivyo alimsaidia kumuingiza switch records kunoa kipaji chake.

Kazi yake ya kwanza anasema ilikuwa ni ‘Bilima’ ya Nuh Mziwanda, huku akieleza kuwa mtu aliyemvutia kuingia kwenye tasnia ya u-producer ni Producer Majani.

Nisikusimulie kila kitu PLAY video umsikie mwenyewe akifunguka.

Comments are closed.