The House of Favourite Newspapers

VIDEO: JPM ALIVYOMPIGIA SIMU KENYATTA HADHARANI

RAIS John Magufuli leo Jumatano,  Julai 24, 2019,  amempigia simu Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, hadharani ambapo wawili hao wamezunguza na kusikika kwa watu wote waliokuwa wakifuatilia tukio hilo.

Mazungumzo ya marais hayo yalikuja baada ya kushuhudia makabidhiano ya dhahabu na fedha iliyokamatwa nchini Kenya mwaka 2004,  iliyowasilishwa na mjumbe maalum wa Rais wa Kenya, Kenyatta, Waziri wa Mambo ya Nje Kenya, Monica Juma,  Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya maneno waliyoongea viongozi hao ni yafuatayo:

JPM- Nashukuru Rais Kenyatta, dada yangu Monica ameniletea mzigo wote wa dhahabu ninao hapa.

KENYATTA-Asante sana, nilisema mali za wananchi wa taifa lingine hatuwezi kuzitumia, sisi ni ndugu tuendelee kushirikiana, amani tuliyopewa tutailinda.

JPM- Nilikuwa nawaambia watu kuhusu huu mzigo kama tungekuwa watu wabaya hizi dhahabu na pesa wasingeziona kabisa.

KENYATTA – “Wananchi wana imani kubwa,  na sisi ni jukumu letu kulinda mipaka na raslimali za nchi zetu,  sisi ni wamoja.

JPM- Ninashukuru sana ulivyomtuma waziri Monica mbali ya kuwa ni mzuri lakini anachapa kazi na anawakilisha vizuri Kenya.

KENYATTA – Wewe achana na huyo,  arudi nyumbani salama.

Kwa habari zaidi fungua video hapa chini.

Comments are closed.