The House of Favourite Newspapers

Vodacom kupeleka mashabiki wa Taifa Stars Misri

Tukielekea msimu wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika (AfCON), kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC, leo imezindua kampeni ya Data na AfCON kupitia huduma ya Soka Letu na itawazawadia wateja kumi wa Kampuni hiyo tiketi za kwenda kushuhudia timu ya Taifa Stars ikicheza huko Misri. Kampeni hiyo ilizinduliwa katika ofisi za makao makuu ya Vodacom jijini Dar es Salaam.

 

Kampeni hii itaendeshwa nchi nzima ili kutoa fursa kwa kila mtanzania na shabiki wa Taifa Stars kushinda.

 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara wa Vodacom, Bi. Linda Riwa, alisema huu ni wakati wa kusapoti vya nyumbani. “Tunafuraha kubwa kuona timu yetu ya taifa imefuzu kuwania kombe hili la AfCON, na tunasambaza furaha yetu kwa wateja wetu. Kama mnavyojua kwa takribani miaka 39 timu ya taifa haikupata fursa ya kuwania mashindano haya, hivyo inabidi tuipe nguvu na kuishabikia. kupitia huduma ya Soka letu kutoka Vodacom Tanzania tutawazawadia wateja wetu 10 ambao ni mashabiki wa Taifa Stars tiketi za ndege pamoja na malazi huko Misri ili wakaishangilie timu yetu ya taifa”

 

Alitaja kuwa kampeni hiyo inaanza rasmi leo, tarehe 7 Juni na kufungwa tarehe 21 Julai ambapo washindi watatangazwa. “Kuna zawadi kemkem katika msimu huu wa kombe la mataifa ya Africa kupitia Data na AfCON, hivyo ili ushinde inabidi ujiunge na huduma ya Soka Letu kwa kubonyeza *149*84# na utapokea jumbe mbali mbali kuhusiana na mechi zinazoendelea. Na si hayo tu, kutazama mechi mbashara unahitaji kuwa na intaneti ya uhakika hivyo endelea kujiunga na vifurushi vya intaneti upate hadi mara mbili ya kifurushi unachonunua “Data Datani” Aliongeza Bi Riwa.

 

Kwa Wateja wapya, watapata dakika tano bure za kupiga papo hapo, lakini pia Wateja wote wanaweza kujishindia Dk 10,000 za kupiga kutoka Vodacom Tanzania PLC, na pia watapata nafasi ya kujibu maswali na kujishindia point nyingi zaidi, point hizi zitawawezesha kuingia katika droo ambayo washindi watapata tiketi za kwenda Misri huku gharama zote zikiwa zimelipiwa na kampuni hiyo

 

Wateja wa Vodacom pia wanaaswa kufuatilia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, kila Taifa Stars itakapocheza na kushinda, kutatolewa namba maalum ambazo mteja akiingiza katika simu yake atajishindia zawadi mbalimbali.

 

“Tuna Zawadi nyingi na za aina mbalimbali, nawaomba wateja wetu waendelee kufuatilia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, hiii itawawezesha kujishindia kila tutakapokuwa tunatoa zawadi,” alisema Riwa huku akiongeza kwamba kwa kila goli litakalofungwa wateja wa Vodacom watajipatia dakika za bure na kuwaasa watembelee kurasa hizo ili kujua namna watakavyojishindia dakika hizo.

 

Nao washabiki wa Taifa Stars Juma Hamisi wa Mbagala na Christian John wa Mwenge wameipongeza kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC kwa kuwa wadau wakubwa wa soka nchini. “Tunafurahi sana kuona Vodacom wakitusapoti kwa hili, nina imani washindi watakaopatikana wataongeza ushabiki kule Misri na kututia nguvu ya kufanya vizuri katika msimu huu,” alisema bwana Hamisi.

 

“Vodacom Tanzania PLC tunajivunia muitikio mkubwa tunaoupata kutoka kwa wateja wetu mbali mbali, ndio maana tunaendelea kuleta huduma na bidhaa nyingi zaidi. Huduma ya Soka letu ilizinduliwa mwaka 2018 na mpaka sasa kuna wateja wetu wengi wanatumia huduma hii kupata taarifa mbalimbali zinazohusu soka, hivyo nawasihi wateja wetu waendelee kujiunga ili wapate dondoo za AfCON,” alihitimisha bi. Riwa.

Comments are closed.