The House of Favourite Newspapers

Vodacom Yasherehekea Miaka 10 Ya Mafanikio Ya M-Pesa Nchini

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao.

 

KAMPUNI  ya Simu ya Vodacom Tanzania imefanya hafla fupi ya kusherehekea na kuadhimisha mafanikio ya miaka kumi ya huduma yao ya M-PESA iliyosambaa nchi nzima. Maadhimisho hayo yamefanyika makao makuu ya kampuni hiyo yaliyoko  eneo la Morocco jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom,  Ian Ferrao, pamoja na kuwapongeza Watanzania kwa ushirikiano wao, amesema huduma hiyo ya M-Pesa iliyozinduliwa mwaka 2008 imechangia kukua kwa uchumi kwa watumiaji kutumia huduma hiyo kufanya malipo ya vitu mbalimbali, na kupokea pesa kutoka kwa mtu yeyote aliyeko popote ndani ya Tanzania na nje ya nchi.

Ferrao  akimkabidhi mmoja ya wadau wa M-Pesa tokea ilipozinduliwa.  Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia.

Mworia akiongea na wanahabari (hawapo pichani).

Aidha, mkurugenzi huyo amesema kuwa kupitia M-Pesa kwa sasa mtu anaweza kulipia huduma mbalimbali kama za ving’amuzi, huduma ya maji, huduma ya luku, marejesho ya mikopo,  huduma za elimu, bima, kununua vifurushi na vocha, kutoa na kuweka pesa benki na kutuma pesa mitandao mingine.

Comments are closed.