The House of Favourite Newspapers

VODACOM, Doris Mollel Foundation WATOA MIL 25 KUSAIDIA HOSPITALI YA RUFAA DODOMA

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kulia mwenye mkoba) akizungumza kwenye hafla hiyo. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation Rosalynn Mworia akifuatiwa na  Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel. 

KATIKA kuunga mkono lengo la serikali la kupunguza vifo vya uzazi na watoto njiti ili  kupunguza uwiano wa vifo vya uzazi hadi kufikia watoto 292 kati ya  watoto 100,000 kwa vizazi hai kutoka watoto 556 kati ya 100,000, Vodacom Tanzania Foundation ikishirikiana na Doris Mollel Foundation imetoa mchango wenye thamani ya Sh. milion  25 milioni kwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma ili kulinda maisha ya watoto njiti.

 

Tukio hili lilishuhudiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Waziri wa Madini, Angellah Kairuki, na Antony Mavunde Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu anayesimamia Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na walemavu.

Mworia, akikabidhi mashine ya kusaidia kupumua kwa watoto njiti kwa  Kairuki (wa pili kulia). 

Msaada wetu unajumuisha vifaa muhimu vya kuokoa maisha kama vile vifaa vya oksijeni (Oxygen concentrator) ambavyo vitasaidia watoto njiti kupumua, themometa 10, mashine  nne za kupimia watoto, mashika 40, mashine tatu za kuwapa watoto joto, mashine tatu za kusaidia kuzalishia, vifuniko vya nyuso na mipira ya kulishia watoto 1,000, mashine ya kuchukulia picha za mwili,  na vitanda vitatu vya watoto.  Mchango kama huo pia utawasilishwa katika Kambi ya Wakimbizi iliyoko Nyarugusu Mkoani Kigoma.

 

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano  wa  Vodacom, Bi Rosalynn Mworia alisema, “Vodacom imeazimia kupunguza idadi ya vifo vinavyotokea wakati wa kujifungua pamoja na vifo vya watoto wachanga na inaunga mkono jitihada za serikali za kuboresha utoaji wa huduma za afya. Tunatarajia kwamba mchango wetu utaenda mbali katika safari nzima ya kuokoa maisha mengi zaidi ya wanawake na watoto. ”

Afisa Muuguzi Msaidizi kutoka Kitengo cha Kuhudumia Watoto Njiti, Constancia Mankupe akizungumza jambo. Kulia  ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayesimamia Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na walemavu Anthony Mavunde. 

 

Kwa upande wake,  Mwalimu alisema, “Mpango huu unakuja wakati muafaka ambapo serikali imeanza kampeni ya kupunguza idadi ya vifo vya akina mama wakati wa kujifungua na watoto wachanga hapa nchini. Tunapenda kuwashukuru Vodacom Foundation na Doris Mollel Foundation katika kusaidia nchi kukabiliana na changamoto hizi. Vifaa hivi cheza nafasi muhimu katika kukabiliana na matatizo ambayo watoto njiti hukutana nayo hasa katika wiki nne za kwanza za maisha yao.”

 

Alitoa wito kwa wafanyakazi wa afya kuhakikisha matumizi sahihi ya vifaa vya kuokoa maisha ya watoto njiti akisema, “Ninawasihi wafanyakazi wa afya katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kutumia kwa usahihi vifaa hivi. Msiruhusu mashine zikusanye vumbi, mashine hizi ziko hapa kwa ajili ya kuokoa maisha ya Watoto wetu. ”

 

Pia alikuwepo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge ambaye alisema kupambana na vifo vya watoto wachanga nchini Tanzania ni suala mtambuka, maana ni wajibu wa kila mmoja wetu kwa pamoja.

“Mchango huu ni ishara kubwa ya ushirikiano kwa kampeni inayoendelea, Jiongeze – Tuwavushe Salama na inalingana na kiapo nilichochukua, pamoja na Wakuu wengine wa Mikoa, ambapo tuliahidi kufanya kazi ya kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga nchini Tanzania  kwa mujibu wa mkakati husika wa serikali chini ya Wizara ya Afya, ” alisema.

 

Kwa upande wao, Kairuki, na  Anthony Mavunde, waliihimiza Vodacom Tanzania Foundation kuendelea na jitihada za kusaidia wanawake na wasichana nchini kote kuboresha afya zao, kupata elimu bora na kubuni miradi mipya.

Comments are closed.