The House of Favourite Newspapers

Simba Yatoka Sare na Mtibwa, Uwanja wa Jamhuri Morogoro

simbanamtibwa

Dakika 90: Mpira Umekwisha, Simba wanatoka 0-0 na Mtibwa Sugar.

Dk 90+ 2: Simba wanapata faulo kwenye lango la Simba, wanacheza fyongo mpira unatoka nje ya lango la Mtibwa.

DAKIKA 4 ZA NYONGEZA

Dk 89, Mtibwa wanafanya kazi ziada kuokoa mpira wa faulo
Dk 86, Kipa Mohammed anafanya kazi ya ziada na kuugusa mpira uliokuwa unajaa wavuni, kona. Simba wanachonga lakini haina madhara

Dk 85: Mtibwa wanafanya mabadiliko hapa, hussein Javu anaingia kuchukua nafasi ya Jaffary Salum.

Dk 84: Simba wanafanya mabadiliko hapa, Mnyate anaingia kuchukua nafasi ya Kichuya.

D 81, Nafasi nzuri kwa Mtibwa, mabeki wa Simba wanagongana na mpira unamkuta Friday, lakini anapinga shuti matege….hakuna kitu
Dk 79, Mandawa tena, anaachia mkwaju mkali lakini anapaisha juuu

Dk 77: Mtibwa wanafanya mabadiliko hapa, Kelvin Friday anaingia kuchukua nafasi ya Vicent Barnabas.

Dk 75: Refa anaonekana kuzozana na benchi la ufundi la Mtibwa Sugar.

Dk 73: Mandawa anaingia, anamuangalia kipa na kupiga bonge la shuti lakini anakosa bao hapa. Mabeki wa Simba wanaonekana kutegeana hapa. Jambo ambalo linaweza kuwasababishia madhara endapo Mtibwa wakitumia mapungufu hayo.

Dk 70: Simba wanakosa bao hapa, Mwanjali anajikunja nje ya 18 lakini anakosa bao.

Dk 68, Kichuya anawachambua mabeki wa Mtibwa lakini Shomari anatoa na kuwa kona, inachongwa na kuokolewa

Dk  65 Baba Ubaya anagongana na Hamad Juma na wote wako chini wanatibiwa

KADI Dk 64, Issa Rashid “Baba Ubaya” analambwa kadi yah njano kwa kumuangusha Kazimoto

Dk 59, Kichuya anamtoka Baba Ubaya, krosi safi kabisa lakini Mbonde anaruka na kupiga kichwa safi kabisa

Dk 57: Kichuya anajaribu kumtafuta ajibu lakini mpira unakuwa mwingi unatoka nje.

Dk 57, Liuzio anamzidi mbio Henry lakini anashindwa kuudhibiti mpira kutokana na uwanja kuwa mbovi
Dk 54, Simba wanamuingiza Ajibu kuchukua nafasi ya Mavugo

DK 52, Simba wanakosa bao la wazi tena hapa. Wanaonekana kurudi kwa kasi kweli kweli.

Dk 50, Mpira bado unakuwa ni wa kubutua zaidi lakini safu ya ulinzi ya Simba wanapaswa kuwa makini hasa pembeni

DK 45, Mtibwa wanaanza kwa kasi, krosi nzuri ya Barnabas nakuwa kona

Dk 45: Mpira ni mapumziko bao ni 0-0.

Dk 41; Mavugo anageuka na kuachia fataki hapa, linatoka kidogo juu la lango la Mtibwa

Dk 38; Mavugo anakosa bao la wazi kabisa, amefanya maamuzi ya haraka kupiga angetulia angefunga. Luizio na Kotei wanafanya kazi nzuri hapa, wanagongeana vizuri lakini shuti la Mavugo linashindwa kulenga

Dk 31 Kotei anafanya anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira miguuni mwa Chanongo akiwa anakaribia kuachia fataki karibu na lango la Simba. Inakuwa kona, inachongwa na Issa Rashid lakini Simba wanaokoa

Dk 29, Luizio anamtoka Ali Shomari, anapiga krosi safi kwa Mavugo akiwa yeye na kipa Mohammed lakini anashindwa kufunga

Dk 28, Method Manjali anacheza mpira wa adhabu kuelekea Mtibwa lakini mpira unakuwa ni mwingi.

Dk 24 Kichuya anamchezea faulo Shaban Nditi, tayari Mtibwa wamekwishaanza hapa, lakini wanaonekana kushindwa kuumudu mpira wanapoteza.

Dk 20, hakika mpira hauna mvuto sana. Mtibwa Sugar wanapata kona, inachongwa vizuri na Mandawa anapiga kichwa safi kabisa, lakini Agyei anadaka vizuri

Dk 15, Kotei mita 28 anaachia shuti kali lakini Said Mohammed anadaka vizuri kabisa. Simba wanaonekana kutokuelewana, hali kadharika hata Mtibwa pia.

Dk 14, Mtibwa Sugar wanafanya shambulizi kali hapa, lakini Simba wanaokoa na kuwa kona. anaichonga Baba Ubaya lakini Simba wanaokoa vizuri

Dk 9: Timu zinacheza kwa tahadhari kubwa wakiogopa kufungwa magoli ya mapema.

Dk 6, Simba wanapata kona, anaichonga hapa Kichuya lakini ni kona hovyoooo
Dk 4 mpira safi wa krosi wa Hamad Juma lakini unakosa mtu, Mtibwa wanaokoa

Dk 1: Mtibwa wanaanza kugusa, mechi imeanza hapa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Moogoro, lakini ikionekana kuanza kwa kubutua. Mtibwa wanapata faulo si mbali na lango la Simba

KIKOSI MTIBWA:
1-Said Mohamed
2-Ally Shomary
3-Issa Rashid
4-Henry Joseph
5-Salim Mbonde
6-Shaban Nditi
7-Haruna Chanongo
8-Ally Makarani
9-Rashid Mandawa
10-Jaffary Salum
11-Vicent Barnabas
SUB
-Benedict Tinoko
-Rogers Gabriel
-Kassian Ponera
-Dickson Daudi
-Ibrahim Rajabu Jeba
-Kelvin Friday
-Hussen Javu
KIKOSI SIMBA:
1. Daniel Agyei,
2. Hamad Juma,
3. Mohamed Zimbwe
4. Abdi Banda
5. Method Mwanjale,
6. Jonas Mkude
7. Shiza Kichuya
8. James Kotei
9. Laudit Mavugo
10 Juma Liuzio
11. Mwinyi Kazimoto
Sub…
Peter Manyika
Novatus Lufunga
Jamal Mnyate
Pastory Athanas
Mzamiru Yassin
Ibrahim Ajibu

Comments are closed.