The House of Favourite Newspapers

VUNJA BEI WANAGAWA TU VYOMBO, UKISOSA NI UZEMBE WAKO!

Mwanamichezo Vunja Bei ameamua kuhakikisha watu wanapata vyombo vya ndani kwa bei nafuu akitengeneza ofa mbalimbali.
 
Mambo ni moto! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kujipatia zawadi mbalimbali kutoka kwa mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Shija Ulaya ‘Vunja Bei’ katika promosheni ya vyombo vya nyumbani inayoendelea kufanyika katika Kituo cha Mafuta cha Big Bon kilichopo Sinza Mori.
Kama unahitaji vyombo vya nyumbani na vilivyo bora kabisa, basi tembelea katika kituo hicho ambapo ukinunua chombo kimoja unapata na vingine bure lakini pia kwa wale wenye magari, bajaj, pikipiki pia watajipatia zawadi kutoka kwa mfanyabiashara huyo endapo tu watajaza mafuta katika kituo hicho cha Big Bon.
Akizungumzia promosheni hiyo, Vunja Bei alisema kuwa lengo kubwa ni kuwawezesha Watanzania wote kupata vyombo vya nyumbani vilivyo bora kabisa kwa matumizi ya binadamu tena kwa bei poa kabisa.
“Promosheni kama hii tumekuwa tukiifanya sehemu mbalimbali hapa nchini lengo likiwa ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata vyombo bora vya nyumbani kwa gharama nafuu kabisa.
“Kwa hiyo niwaombe tu watu wote ambao wanahitaji vyombo bora kabisa vya nyumbani wafike hapa Big Bon ambapo akinunua kimoja anapata vingine bure au kwa wale watakaonunua mafuta katika kituo hiki pia watapata zawadi ya vyombo bure kabisa,” alisema Vunja Bei.

Comments are closed.