The House of Favourite Newspapers

Wabunge wa Yanga kutifuana na wa Simba

ngereja1

Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Ilala,  Mussa Zungu, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na Mbunge wa Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda wote wakiwa wachezaji wa timu ya bunge.

ngereja2

Ngeleja akifafanua jambo mbele ya wanahabari.

ngereja3

Baadhi ya wasanii wa timu za Bongo Muvi na  Bongo Fleva (waliosimama nyuma) wakiwa katika mkutano huo.

ngereja4

Mbunge wa timu ya Yanga bungeni, Salim Turki ‘Mr White’ ambaye ni mbunge jimbo la Mpendae akielezea jinsi walivyojipanga katika timu yake.

ngereja5

Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano huo.

ngereja6

Msanii wa Timu ya Bongo Muvi, Single Mtambalike  ‘Richie Rich’ akielezea jinsi walivyojipanga kuwapiga wasanii wa Bongo Fleva.

ngereja7

Msanii wa Timu ya Bongo Fleva, Karama Masoud ‘Kalapina’ (wa pili kushoto) naye akielezea walivyojipanga.

JUMAPILI ya Septemba 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kutakuwa na mchezo maalum wa soka ambao utawakutanisha wabunge ambao ni wapenzi wa Yanga dhidi ya wale wa Simba ikiwa ni mahususi kwa ajili ya kukusanya fedha zitakazowasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea Septemba 10 mwaka huu  mkoani Kagera.

Katika mchezo huo, viingilio vitakuwa ni Sh 3,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, Sh 10,000 na 15,000 itakuwa kwa ajili ya viti vya rangi ya machungwa huku Sh 50,000, 100,000 na 200,000 ikiwa ni kwa V.I.P C, B na A.

Lakini kwa viti 50 pekee maalum vitakavyokuwa karibu na mgeni rasmi wa mechi hiyo ambaye atatajwa baadaye, kila kimoja kitalilipiwa Sh 1,000,000.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bunge SC, William Ngeleja, ameeleza kuwa mbali na mechi hiyo kutakuwa pia na mechi za baina ya Bongo Muvi Vs Bongo Fleva, timu ya netiboli ya bunge itaumana na ile ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), lengo likiwa ni kukusanya fedha nyingi zaidi za kuwasaidia waathirika wa tukio hilo.

“Lengo letu ni kukusanya fedha za kuwasaidia ndugu zetu wa kule Kagera, angalau warejewe na hali waliyokuwa nayo awali, tangu awali kule bungeni kupitia posho zetu tulishachanga milioni 85 lakini tunahitaji kuongeza zaidi misaada kwao ndiyo maana tumeandaa mechi hii ili kila Mtanzania kupitia kiingilio alichonacho naye ashiriki kuwakomboa ndugu zetu hawa.

“Vikosi vitakuwa vikali kwa ajili ya kutoa burudani ya kutosha, huku kwetu Simba tutakuwa na Kassim Majaliwa, Hamis Kigwangwala, Kaizer Makame na wengine. Kule Yanga nao watakuwa na Ridhiwani Kikwete, Anthony Mavunde, Mwigulu Nchemba na wengine wengi.

“Bongo Muvi wao watakuwa na kina Ray Kigosi, JB, Muhogo Mchungu, Dk. Cheni na wengine, lakini Bongo Fleva wao watakuwa na kina Tundaman, Ali Kiba, Diamond, KR Mullah na wengine. Kuhusu mgeni rasmi, tunakamilisha taratibu na muda si mrefu tutamtangaza,” alisema Ngeleja ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema.

Comments are closed.