The House of Favourite Newspapers

Wadau wa Uvuvi Bahari Kuu Wawasilisha Maoni Kuhusu Swiofish

0
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Fatuma Sobo (aliyesimama) akijadiliana na wadau.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu Tanzania, Dk. Omary Ali Amir akizungumza na mtandao huu.
Baadhi ya wadau waliohudhuria mkutano huo.

MAMLAKA ya Uvuvi wa Bahari Kuu na wadau kutoka taasisi mbalimbali, zikiwemo Wizara za Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Bara) na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi (Zanzibar) wamekutana na kutoa mchango wa maoni yao juu ya mkakati wa mawasiliano wa SWIOFish, ikiwa ni pamoja na kutoa pendekezo la marekebisho.

Akizungumza na mtandao huu baada ya kumalizika kwa mkutano huo leo jijini Dar ws Salaam, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu Tanzania, Dk. Omary Ali Amir, amesema lengo la kukutana kwao ni kuona kama kuna maeneo yanayohitajika kurekebishwa juu ya waraka maalum uliotolewa ukiwa na mapendekezo ya mradi huo kama yalivyowasilishwa na mwelekezi wa mradi huo. Iwapo maoni ya wadau yatakuwa muhimu, yatafanyiwa kazi.

“Tumeamua kukutana na wadau na taasisi mbalimbali, wakiwemo pia wenzetu wa Wizara za Kilimo na Uvuvi kutoka Bara na Visiwani kwa maana hiyohiyo moja ya kutoa maoni na mapendekezo yetu juu ya mikakati ya kimawasiliano (communication strategies) kama ambavyo nyaraka ilivyotolewa na msimamizi mwelekezi, baadaye kitaitishwa kikao cha waratibu na kupitia mapendekezo hayo kabla ya maoni hayo kupelekwa kwa hatu zingine zaidi,” alisema Dk. Omary Ally Amir.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply