The House of Favourite Newspapers

Wadudu 7 Wenye Uerevu, Ufahamu Zaidi Duniani

Miongoni mwa wadudu wengi duniani, wapo wadudu kadhaa wanaoeleweka kirahisi kwa binadamu, ambao wana uerevu unaoonekana kwa binadamu au uliofichika lakini ukaonekana kwa vitendo vyao.  Wafuatao ni wadudu saba wenye uerevu zaidi.

1. Nyuki
Hawa wanaeleweka kirahisi katika kazi zao za kutengeneza moja ya vitu vitamu zaidi duniani — asali.  Ushirikiano wao uko wazi kwa binadamu.

2. Vunjajungu
Wanaofuga wadudu hao, wanasema ni rahisi kuwafundisha tabia fulani, ikiwa hata kutoa sauti za kubusu (kiss)!

3. Nzige
Hawa wanaweza kutoa sauti za kila aina kuambizana iwapo kuna chakula mahali fulani au kutoa ilani za hatari.

4. Vipepeo
Ni wapesi wa kujua rafiki na adui.  Ni wapole, hususan kwa kutambua kwao kwamba binadamu si adui yao.

5. Sukuma Kinyesi (Dung Beetle)
Ana uwezo wa kufahamu maeneo ya kufika na kufikisha mzigo wake hata katika mazingira magumu. Hakati tamaa.

6. Mchwa
Ushirikiano wao, kufahamu pande zozote na mazingira ya mvua, jua na kadhalika ni mambo yanayoonyesha uerevu wao unaokwenda sambamba na kazi zao.

7. Mende
Pamoja na kuchukiwa na binadamu wana uwezo wa kuishi mahali popote katika mazingira yoyote, mradi pawe pana chakula tu.  Ni wepesi kukimbia na kumtoroka adui na kujificha asionekane, hata kama adui akiwa karibu.

 

 

 

 

 

Comments are closed.