The House of Favourite Newspapers

Wafanyabiashara 6 Kizimbani Tuhuma za Kuhujumu Uchumi

0

WAFANYABIASHARA sita leo Februari 25, wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi likiwemo kosa la utakatishaji fedha zaidi ya shilingi bilioni 4.

 

Washitakiwa hao ni Baraka Madafu, Mark Mposo,Lusekelo Mbwele, Leena Joseph, Bernard Mndolwa na Salvina Karugaba wote  wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambapo wamesomewa mashitaka yao na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi, akisaidiwa Waknyo Simon Wakili Mwandamizi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Cassian Matembele.

 

Katika shitaka la kwanza wakili wa serikali mwandamizi Wankyo Simon amedai kuwa katika tarehe tofauti kati Desemba 4, 2018 na Decemba 31 mwaka 2020 mshitakiwa Baraka Madafu na wenzake waliongoza genge la uhalifu nakujipatia zaidi shilingi bil. 4 kutoka Benki ya NBC Tawi la Masaki lililopo Jijini Dar es Salaam kwa njia ya udanganyifu.

 

Katika shitaka la pili Wakili Simon wamedai kuwa katika tarehe tofauti kati ya Februari 6 mwaka 2019 maeneo ya Masaki Jijini Dar washitakiwa hao walighushi nyaraka ya uongo ya mkataba wa Benki wakionyesha kuwa watu sitini ambao ni waajiriwa wa Kampuni PEERTECH LIMITED ni wanufaika wa mkataba huo wakati wakijua sio kweli.

 

Aidha katika shitaka la tatu hadi la kumi na moja ambayo nayo ni ya kughushi nyaraka na utakatishaji Wakili wa Serikali Mkuu Paul Kadushi na Waknyo Simon wamedai washitakiwa hao katika tarehe tofauti mwaka 2019 na mwaka 2020 walighushi nyaraka ya kujipatia mkopo kupitia Benki ya NBC tawi la Masaki wakionyesha watu sitini kutoka Kampuni ya PEERTECH LIMITED ni wanufaika wa mkopo huo wakati wakijua sio kweli.

 

Baada ya maelezo hayo washitakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

 

Wakili wa Serikali Mkuu Paul Kadushi amedai upepelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa, kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 12,2021 kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande.

Leave A Reply