The House of Favourite Newspapers

Wafanyakazi NBC Watoa Elimu ya Fedha Kwa Wanafunzi Dar

Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Toivo Mapunda (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa kuhusu elimu ya fedha, ujasiriamali na stadi za maisha wakati yeye na wafanyakazi wenzake walipotembelea shuleni hapo jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.
Mmoja wa maofisa wa benki ya NBC, Isaya Komba (kulia), akitoa elimu ya masuala ya kifedha, ujasiriamali na stadi za maisha kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa ikiwa ni sehemu ya majukumu ya kujitolea katika kuisaidia jamii yanayofanywa na wafanyakazi wa NBC sehemu mbalimbali nchini.

Mkuu wa Kitengo cha Mikopo cha Makampuni wa Benki ya NBC, Elibariki Ndossi (kushoto), akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa kuhusu elimu ya kifedha, ujasiriamali.

Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa akiuliza swali katika hafla hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.
Meneja Mahusiano Msaidizi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa kuhusu elimu ya fedha, ujasiriamali na stadi za maisha. 

Comments are closed.