The House of Favourite Newspapers

WAHITIMU UDSM KUTIMUA MBIO ZA HALF MARATHON

Kutoka kushoto ni Dkt. Lulu Kaaya, Balozi Maajar na Profesa David Mfinanga wakizungumza na wanahabari.

Kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa David Mfinanga leo aliwakaribisha wanahabari katika Kampasi ya Mwalimu J.K Nyerere Mlimani na kuwaeleza nia ya umoja wa waliowahi kuhitimu chuo hicho, kuanzisha mbio za Half Marathon kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa kituo cha wanafunzi kwa ajili ya shughuli zao za kimasomo.

Akizungumzia mbio hizo, Mkurugenzi wa Jumuiya hiyo Dkt. Lulu Kaaya amesema mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Desemba 7 mwaka huu na kuwaomba wadau wajitokeze kushiriki mbio hizo zenye lengo la kuchangia ujenzi huo.

Dkt. Kaaya amesema mbio hizo zitakuwa endelevu na kufanyika kila mwaka. Naye Rais wa Jumuiya hiyo, Balozi Mwanaidi Maajar aliwaomba wahitimu wa chuo hicho popote walipo wajitokeze kushiriki mbio hizo zenye lengo la kujenga afya zao na kufanikisha ujenzi wa kituo hicho.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL      

Comments are closed.